mjasiliaupeo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2013
- 2,162
- 3,086
Najua sio mgeni wa neno tajwa hapo juu "Kwenye kichwa cha habari" kama umeshawahi kutembelea mitandao ya jamii, haswa mtandao wa Instagram. Neno hili na mengineyo kama "Follow uone Diamond alivyokuwa anamgonga Wema" au "follow uone uthibitisho wa DNA inayoonyesha tiffah sio wa Dai" hutumika kujipatia followers wengi zaidi katika page zao. Sasa unaweza ukajiuliza hawa watu wanapata faida gani? kuna wakati na mimi nilijiuliza swali kama hilo na kujaribu kufanya kauchunguzi kwa maana sio rahisi kwa mtu kukesha kwenye mitandao ya jamii kufanya jambo kama hilo bila faida, tena kwa kuweka comment zenye ulaghai"zisizo na ukweli" nikagundua kitu.
1. Hawa watu wanaziuza account zao kwa wafanyabiashara, yaani account ikifikisha followers 100k inaweza kughalimu mpaka tsh 300,000/= hadi 500,000/= na hawa vijana ambao tunawaona kama wapuuzi flani wanamiliki hata tano kwa wakati mmoja.
2. Wengine wanatumia kufanyia matangazo ya biashara, yaani unalipa kiasi cha pesa alafu wanakutangazia biashara yako. Hizi ni accounts ambazo zina followers angalau kuanzia 300k na kuendelea, nilijaribu kuwasiliana na mmoja kipindi flani na hayo ndio majibu yake(pitia bandiko la picha juu) Anabandika bandiko moja la biashara katika ukurasa wake kwa Tsh 40,000/= mawili kwa 70,000/= na nikajaribu kumdodosa na kufuatilia ukurasa wake nikajiridhisha ya kuwa anabandika si chini ya matangazo kumi kwa siku, kwa tafsili rahisi ni kuwa anaingiza si chini ya laki nne kwa siku(400,000) inastaajabisha sana...
NB; kuna njia nyingine ambayo wanaitumia kujiongezea followers, hii ni kuunga mkono kundi flani katika mtandao wa jamii ili watu wanaompenda mwanamuziki au msanii flani wakufollow. hii pia imewaongezea mtaji wa followers.
Pia kuna njia ya kutengeneza kurasa ya kuchamba, waTanzania wanapenda sana umbea na kuchambana kuliko kitu chochote kwenye mtandao wa kijamii, hawa watu wanaochamba wenzao wanapata sana deal za matangazo kwa sababu wao hawana shida sana ya kupata followers, hii inatokana na kuwa katika kila post yao, wapenda michambo wanawatag na kuwa mention wenzao.
Hivi ndivyo vijana ambao hawajaenda darasani wanavyoingiza pesa nyingi kuliko waajiliwa wenye Masters, NIMEJIFUNZA KUTODHARAU UJINGA WA MWENZANGU, KUANZIA LEO NTADHARAU UJINGA WANGU TU... PERIOD!