Unataka kuita mizimu? Fuata njia hii...

Unataka kuita mizimu? Fuata njia hii...

mudy92

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
671
Reaction score
535
Mizimu ni roho za wazee wetu (wa ukoo) toka katika pande zote mbili Baba na Mama ambao ni babu na bibi toka kwa baba na babu na bibi toka kwa Mama,roho hizi huja na kuwa na sisi pale tunapozihitaji au zinapotuhitaji....!

kwanini Mizimu huja kwetu au kwaini tunaiita?
-UDUGU, kumbuka roho hizi ni zile za waze wetu (ancestors) ambao walizaa baba na mama zetu hivyoo kuja au kuwaita hutokana na Udugu
-ULINZI, roho zote zisizo na mwili huona yasiyoonekana kama Uchawi na magonjwa hivyoo Wazee wetu huja na tunawaita watuambie haya tusiyoyaona.
-MILA, utamaduni na desturi zetu hututaka tufanye mambo yaliyo katika mpangilio ulio sahihi kama kuwapa wazee heshima na kusikiliza yale wanayotuambia.

Njia ya Kuwaita Wazee wako (MIZIMU) ili waje kwako na wakuambie utakalo Uliza...

Hatua ya 1.
-Pika POMBE ya ulezi au Pombe yeyote ya Kienyeji itokanayo na nafaka ( Uliza kufahamu babu na bibi yako walikuwa wanakunywa Pombe ipi enzi za uhai wako au wanakunywa ipi kama wako hai.)

Hatua ya 2.
-Tafuta KUKU mweupe kabisa asiye na Doa wakienyeji chinja na Muache afe kwa Kurukaruka mpaka atakapo kata Roho, kisha Mpike kama Mboga

Hatua ya 3.
-pika CHAKULA asili cha wazee wako kama Ugali, Ndizi na Mihogo au pika vyoote kwa Pamoja (usichanganye) katika kiasi kidogo kila chakula ila wali pika Mwingi.

Hatua ya 4.
-karibisha watu kwako waje kula Haswa Watoto na Wazee pia wape Wazee wanywe pombe uliyopika kwako na wakirimu kwa kila kitu, Kama wazee wako walikuwa wafugaji Nunua maziwa ya Pakti na Uwape watoto na wazee wanywee.

KUMBUKA:
1-kuwanawisha watu wote wanaokuja kula kabla na Baada ya Kula.

2-ukikosa Pombe kanunue vilabuni

3-usipikie Vyombo vilivyopikiwa Kitimoto

UTAPATAJE MAJIBU KUWA WAZEE (MIZIMU) WAMEFURAHI NA WAPO TAYARI KUKUSKILIZA?
- wakati wa Kulala Omba Mungu kisha Ita wazee wako woote wa Ukoo kwa baba na Mama kisha waambie shida yako kisha Wao watakuja Ndotoni na Jibu lako....

Jibu linaweza kuwa La mafumbo au Dhahiri Kazi kwako!
 
" Jibu linaweza kuwa La mafumbo au Dhahiri Kazi kwako!"

bado si dhairi!
 
"Wakati wa kulala omba Mungu....." tofautisha Mungu na Mingy,, Usimuhusishe Mungu mizimu
 
Mungu anatambua mizimu ni nini. Unapo omba mizimu yabidi kumtanguliza Mungu kabla ya yote na wote Mungu na mizimu watakusikia. Tatizo unapokuja hapa na imani ya hizi dini za kuletewa (islam na ukristo), mtu anakuja na kanuni zake za upotoshaji.
 
Kwahiyo kama walikua hawanywi pombe...?mkuu usilete habari za uongo
 
Enzi za babu zetu hakukuwa na Dini za kuletewa,waliabudu hiyo mizimu mambo yalikuwa shwari, na hapa kuwa na ukimwi, wachungaji wa mwendokasi au wajasiria mali wanaotumia biblia.. majanga ya kutisha,ndoa za jinsia moja, ugaidi..lakin Dunia ya leo ya watu wanaotambua uwepo wa Mungu ndio imeongeza vitendo viovu kuliko hapo kale..yawezekana ni matokeo ya Dini mpya
 
Hujakatzwa kuabudu mizimu yako MKUU! Sisi tunahubir INJILI NA tunawatoa mapepo yenu waabudu mizimu! Shenzi
 
Mizimu ni roho za wazee wetu (wa ukoo) toka katika pande zote mbili Baba na Mama ambao ni babu na bibi toka kwa baba na babu na bibi toka kwa Mama,roho hizi huja na kuwa na sisi pale tunapozihitaji au zinapotuhitaji....!

kwanini Mizimu huja kwetu au kwaini tunaiita?
-UDUGU, kumbuka roho hizi ni zile za waze wetu (ancestors) ambao walizaa baba na mama zetu hivyoo kuja au kuwaita hutokana na Udugu
-ULINZI, roho zote zisizo na mwili huona yasiyoonekana kama Uchawi na magonjwa hivyoo Wazee wetu huja na tunawaita watuambie haya tusiyoyaona.
-MILA, utamaduni na desturi zetu hututaka tufanye mambo yaliyo katika mpangilio ulio sahihi kama kuwapa wazee heshima na kusikiliza yale wanayotuambia.

Njia ya Kuwaita Wazee wako (MIZIMU) ili waje kwako na wakuambie utakalo Uliza...

Hatua ya 1.
-Pika POMBE ya ulezi au Pombe yeyote ya Kienyeji itokanayo na nafaka ( Uliza kufahamu babu na bibi yako walikuwa wanakunywa Pombe ipi enzi za uhai wako au wanakunywa ipi kama wako hai.)

Hatua ya 2.
-Tafuta KUKU mweupe kabisa asiye na Doa wakienyeji chinja na Muache afe kwa Kurukaruka mpaka atakapo kata Roho, kisha Mpike kama Mboga

Hatua ya 3.
-pika CHAKULA asili cha wazee wako kama Ugali, Ndizi na Mihogo au pika vyoote kwa Pamoja (usichanganye) katika kiasi kidogo kila chakula ila wali pika Mwingi.

Hatua ya 4.
-karibisha watu kwako waje kula Haswa Watoto na Wazee pia wape Wazee wanywe pombe uliyopika kwako na wakirimu kwa kila kitu, Kama wazee wako walikuwa wafugaji Nunua maziwa ya Pakti na Uwape watoto na wazee wanywee.

KUMBUKA:
1-kuwanawisha watu wote wanaokuja kula kabla na Baada ya Kula.

2-ukikosa Pombe kanunue vilabuni

3-usipikie Vyombo vilivyopikiwa Kitimoto

UTAPATAJE MAJIBU KUWA WAZEE (MIZIMU) WAMEFURAHI NA WAPO TAYARI KUKUSKILIZA?
- wakati wa Kulala Omba Mungu kisha Ita wazee wako woote wa Ukoo kwa baba na Mama kisha waambie shida yako kisha Wao watakuja Ndotoni na Jibu lako....

Jibu linaweza kuwa La mafumbo au Dhahiri Kazi kwako!
Kama wazee walikua wacha MUNGU toka babu wa babu na waliamini mizimu,pombe ni dhambi unafanyaje sasa..?
 
Hujakatzwa kuabudu mizimu yako MKUU! Sisi tunahubir INJILI NA tunawatoa mapepo yenu waabudu mizimu! Shenzi
Tena nyie ni wajasiria mali tu mnao tumia biblia..na wagonjwa wenu wa kuigiza nendeni hospital kama mtaponya hata mgonjwa 1.. Miujiza ilikuwa zama za Yesu tu...nyie wasaka Tonge mnarusha matangazo ya biashara sio injili..
 
Enzi za babu zetu hakukuwa na Dini za kuletewa,waliabudu hiyo mizimu mambo yalikuwa shwari, na hapa kuwa na ukimwi, wachungaji wa mwendokasi au wajasiria mali wanaotumia biblia.. majanga ya kutisha,ndoa za jinsia moja, ugaidi..lakin Dunia ya leo ya watu wanaotambua uwepo wa Mungu ndio imeongeza vitendo viovu kuliko hapo kale..yawezekana ni matokeo ya Dini mpya
Kwakweli
 
Back
Top Bottom