unataka kufanikiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

unataka kufanikiwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Graph Theory, Apr 10, 2012.

 1. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Lazy men believe in luck, but men of worth believe in facts. A wise man once said, "success is matter of luck, ask any failure". Rather than go for facts, the lazy man thinks people arrived at success by luck. There ia no accidential success, as no accident is a success.
  Kuna watu badala ya kufanya kazi kwa bidii ili wajikwamue kutoka katika umasikini utawakuta wanajadili watu wengine kuhusu mali wanazomiliki. Utawasikia wakisema ni freemason, mara utasikia alitoa mtoto wake kafara na maneno mengine yanayofanana na hayo. Watu kama hao ni watu ambao akili zao naweza sema zimepungukiwa na akili kadhaa, badala mtu afanye kazi kwa bidii, mda wa kazi anautumia kwa kuongelea utajiri wa wengine. Jambo moja kubwa ni kuwa utajiri wa mtu, siri ya jinsi alivyoupata anaijua yeye na Mungu tu, kwa hiyo usipoteze mda wako kukaa katika makundi ya watu waliochoka kiakili kujadili upuuzi kama huo. Utasikia jitu zima na ndevu zake linasema fulani ni freemasonndio maana kapata mafanikio haraka haraka, huu ni ujinga mkubwa, mwache na ufreemason wake na wewe ubaki na mambo yako, maana hapa duniani kila mtu amechagua lifestyle yake, usitake kila mtu Afuate maisha ambayo wewe umechagua. Ni hayo tu ambayo nimeona tushee katika siku ya leo cha mhimu ni kuchapa kazi kwa bidii sana.
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Mkuu ume-hit pale panapotakiwa kabisa. Sisi watanzania tu wavivu sana na wengi wa maneno. Kwa mfano sasa hivi kuna hii kitu inayoitwa freemason-phobia iliyoingia (kimsingi ni ile ile dhana ya zama za kale ya kumwona mtu mwenye maendeleo unamwita mumiani) inaniacha hoi. Wewe ukitaka hata vibaka wasikuibie kwenye gari yako weke lebo ya freemason.... watakuogopa kama jeneza na hakuna atakayekuzoea zoea.
   
Loading...