Unatabiri nini baada ya uchaguzi wa marudio Zanzibar

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Kwa upande wangu naona giza.

Nauona mgogoro mkubwa, kuna hatari ya kuwa na wawakilishi wawili wawili katika kila jimbo na madiwani wawili wawili katika kila wadi. Wote hawa walishakabidhiwa vyeti vya ushindi wao

Naiona hatari ya kuwa na maraisi wawili kwa wakati mmoja. Wote wawili wakiwa na matokeo halali ya ZEC. Mmoja atakuwa na matokeo ya majimbo 54 yaliyotiwa saini na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi wa tarehe 25 oktoba, 2015 pamoja na muhuri wa tume ngazi ya majimbo na mwengine akiwa na matokeo ya tarehe 20 Machi, 2016 yakiwa baadhi ya majimbo hayana saini.

Naona kutumika kwa nguvu nyingi za kulinda utawala utakaomuweka rais chaguo la ZEC wa tarehe 20 machi, 2015

Namuona rais atakayeungwa mkono na jumuiya ya kimataifa kati ya hawa wawili kuwa ndiye atakuwa mshindi wa kweli

Ni utabiri tu wewe unasemaje
 
Blood shed is what makes grass to grow.

Wakati mwengine unaweza kusema kwa nini binadamu wanawaza tofauti -hayo ni maumbile kumbe.

yaani tumejiwekea taratibu zetu wenyewe halafu tunazikiuka kwa ubinafsi wetu. lipi lingekuwa bora kwa huu mzozo wa Zanzibar ' Uchaguzi kwanza au kuondowa sintofahamu'

Naona kile tunachokiogopa ndiyo kinakuja.

Kwa maoni yangu mzozo mkubwa ndio kwanza unakuja
 
Hata mimi naona giza tuu

Na hasa sina hakika ni nini hasa CUF wanawaza na kupanga baada ya wao kuamini kuwa wameporwa haki yao!

Nahisi CUF wanasubiri tu hiki kitu kinachoitwa "uchaguzi wa marudio" wa kesho 20/03/2016 kifanyike halafu mapambano ya kisheria yaanze kujua yupi ni halali, yule aliyechaguliwa kwa uchaguzi wa tarehe 25/10/2015 au huyu wa "marudio" kesho tarehe 20/3/2016??

Hizi pande mbili zinazobishana CUF na vyama vinavyounga mkono upande mmoja na CCM, SMZ na SJMT kwa upande mwingine wote wana hoja zao juu ya hatua ya ZEC kuufuta uchaguzi wa tarehe 25/10/2015 na matokeo yake yote. Upande ukipinga na upande ule ukiunga mkono. Tuone hizo hoja hapa chini;

Hoja ya Jecha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ile ya JMT na CCM ni kuwa Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) ina mamlaka ya kuamua chochote juu ya uchaguzi ikiwemo hata kuufuta wote iwapo inaona kuna sababu za kufanya hivyo zilizo kinyume na sheria ya uchaguzi zimekiukwa.

Na kwa maelezo yao Tume iliufuta uchaguzi wote pamoja na natokeo yake yote na kwa hiyo hawa wadau watatu wa uchaguzi i.e CCM, SMZ na SJMT wanaunga mkono maamuzi ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na ndiyo maana wanashiriki huu uitwao wa marudio kesho.

Ishu hapa ni kuwa, je hoja za ZEC zinajitosheleza kuchukua uamuzi huo? Walikubaliana na kujiridhisha kama ZEC? Nani aweza kuthibitisha hili?

HOJA ya chama kikuu cha upinzani CUF na kinachosema ndicho kilichoshinda uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25/10/2015 ktk ngazi ya urais ni kuwa, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) haina mamlaka ya KIKATIBA na KISHERIA kufuta uchaguzi uliokwishakufanyika na washindi kutangazwa na tume yenyewe!.

Aidha wanasema, matokeo ya uchaguzi yakishakutangazwa sambamba na washindi wake, kisheria anayepaswa kulalamika ni yule aliyeshindwa kama anaona aliyeshinda hakushinda kihalali. Na hili la kulalamika haliwezi kuwa ni jukumu la tume yenyewe ya uchaguzi ambayo mwisho wa siku eti inaamua kufuta uchaguzi na matokeo yake yote!!

Hoja nyingine ya CUF ni kuwa, pamoja na kuwa uamuzi ulikwishafanyika wa kufuta uchaguzi na kuitishwa mwingine "...wa marudio" wa kesho, uamuzi huu wala haukuwa wa Tume bali wa mtu mmoja mwenyekiti wa hiyo tume Bw. Jecha S. Jecha kuanzia kufuta uchaguzi wote wa tar 25/10/2015 na matokeo yake yote pamoja na uamuzi wa kuitisha mwingine "....wa marudio" wa kesho tarehe 20/3/2016 kitu ambacho ni kinyume cha SHERIA na KATIBA!!

Ishu ni kuwa, je ni kweli ni Jecha ndiye aliyeamua kama Jecha ni sio tume nzima kupitia ktk utaratibu wa vikao halali vya tume? Je, ni kweli mwenyekiti hana mamlaka hayo au ni kweli Jecha ni ZEC na ZEC ndiye Jecha? Sheria na katiba zinasemaje? Na je, ni kweli uchaguzi uliokwisha kufanyika na washindi kutangazwa waweza kufutwa!? Nani aweza kututhibitishia haya?
Je, ni ZEC yenyewe? CCM? SMZ? SJMT? au Mahakama??

Kiukweli kama ulivyosema unaona giza, hata mimi naona hivyo hivyo giza nene huko mbeleni.

Naona pia mapambano ya kisheria ya kutambua nani ni kiongozi halali wa kuchaguliwa kati ya huyu atakayechaguliwa kesho wa hiki kinachoitwa "uchaguzi wa marudio" trh 20/3/2016 na yule aliyechaguliwa trh 25/10/2015.
 
Aisee nimeingia Zanj leo hii hali huku tunako elekea mbona shida kutoka tu bandarini nimekutana na wanajeshi wako barabarani wamekuwa matrafic naskia changamka changamka ww dogo.
 
Naona kiza pia.Naona mgogoro utazidi kupanuka na utaendelea mpaka 2020.Mgogoro utatuingiza katika gharama kubwa katika kutetea matokeo ya uchaguzi wa marudio.Idadi ya wapiga kura watakaojitojeza itakuwa ndogo.
 
Naona Jecha salim Jecha akimtangaza Dkt. Alli mohamed Shein kuwa rais Wa Zanzibar......

Maalim Seif anaitisha vyombo vya habari na kudai kuwa ameibiwa kura.....ila hakuna kinachofanyika.....

Polisi na Jwtz wanarudisha vifaa vyao bara baada ya Shein kuapishwa.....

Maisha ya Zanzibar yanakuwa ni yale yale na kila kitu kinarudi ktk hali ya kawaida....
 
MATOKEO Yenyewe, Yanaweza kuwa Hamad Rashid, wa ADC akapata kura nyingi sana (staged votes) , labda akazidiwa asilimia moja hadi tano tu na Rais anaendelea 'na muda wake wa urais' Dkt.Shein. Kisha ukarabati ukafanyika kidogo na anakuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Ametamani sana kumrithi Maalim Seif, na leo fursa imejibainisha! Uchaguzi wenyewe ndio wa hivi, namna hii! Likitokea hili, litakuwa na afadhali zake. Nimeitamani kwa muda mrefu third party kwa Zanzibar (huu ‘U-simba na u-Yanga’, siupendi kivile).

LAKINI MATOKEO pia yaweza kuwa CUF kikapata walau asilimia 40 ya viti vyote vya Uwakilishi, hususan huko Pemba. ZEC yaweza kuwatangaza kuwa washindi. Majina yao yapo yapo kwenye ballot boxes, uchaguzi wenyewe ndio huu wa namna hii. Je watagomea kwenda barazani? Watagoma wote? Inawezekana wakagoma, CUF nawaelewa. Lakini wanaweza kugawika!

Kubwa zaidi ni kwamba mgogoro ndio kwanza unaanza. CUF wanaweza kuwa nje kabisa ya mfumo wa SMZ. Wakajipanga na kujiimarisha zaidi, kuleta ushindani tuendako! Naona KIZUNGUZUNGU TU.
 
Bado ni giza tu. Hapa ndio mwanzo mkoko unaalika mauwa.

Ukiacha hilo la kimahakama na kisheria. Bado mizani ya kimataifa haijajulikana italalia wapi.

Kwa sasa tunajuwa tu kwamba jumuiya ya kimataifa haiungi mkono uchaguzi huu. hatujuwi masindikizo yatakuwaje baadae na mwisho wa ngebe zote unaanzia baada ya tarehe 20 Machi, 2016.

Ninavyojuwa CUf ni wazoefu wa kucheza siasa za Upinzani Tanzania hii hasa Zanzibar jee maamuzi yao ya kususia ni ya bure na hawajujuwa wanachokifanya kiasi cha kumsusia nguruwe shamba la mihogo safari hii?

Nini kitatokea.

Ngoja tuone.
 
Naona Maalim Sefu atashitakiwa kwa uhaini kama miaka ya 90

Bado sio suluhu. Watashtakiwa wengi tu. jee huo utawala wa kuoongoza watu na amani na utulivu itapatikana?

Nchi itavurugika . Ingawa watawala wao hilo wanaliona rahisi kwamba watatumia approach ya FYOKO FYOKO.

Watawala wanachotaka kwa sasa ni kupata uhalali wa kutangazwa na ZEC tu halafu mengine baadae. Wanaamini chochote kitakachokuja wao tayari wana URAISI mkononi.

Acha tuone.
 
hapa wakuu tuhoji gharama za uchaguzi wa marudio,mkumbuke uchaguzi ulishafanyika na kwa gharama kubwa ,haya ni marudio ,hii imekaaje,
 
Bado sio suluhu. Watashtakiwa wengi tu. jee huo utawala wa kuoongoza watu na amani na utulivu itapatikana?

Nchi itavurugika . Ingawa watawala wao hilo wanaliona rahisi kwamba watatumia approach ya FYOKO FYOKO.

Watawala wanachotaka kwa sasa ni kupata uhalali wa kutangazwa na ZEC tu halafu mengine baadae. Wanaamini chochote kitakachokuja wao tayari wana URAISI mkononi.

Acha tuone.
atakae leta vurugu atapigwa kwenye watu laki tano ni rahisi kumdhibiti muovu
 
Back
Top Bottom