Unasema unampenda, unajua thamani ya upendo?

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,320
11,322
‘THERE is no love without sacrifice.’ Hakika kabisa. Hakuna mapenzi bila kujitoa kwa kiwango kikubwa (sadaka).

Napita maeneo ya Kariakoo katikati ya Jiji la Dar, nakutana na kina dada na kina mama wakiwa na mabeseni vichwani mwao. Wanaonekana wako bize kweli kweli. Kila mmoja kwa mwonekano wake anaonekana yuko makini na kila gari na kila mtu anayepita karibu yake.

Wote katika mabeseni hayo wameweka mihogo mibichi na vipande vya nazi. Mmoja anavutia macho yangu zaidi, namuita naye bila hiyana ananisogelea. Anadhani nataka kununua mihogo. Simwangushi; natoa elfu tano na kumpatia. Wakati akiwa bize kumenya muhogo huo, namuomba nimuulize maswali kadhaa huku akiendelea na umenyaji wake. Anakuwa muungwana na kuniruhusu.

Namuuliza kama ameolewa. Anasema ndio, anasema katika ndoa ana miaka mitatu. Akiwa ananieleza hayo naona anakuwa mtulivu zaidi. Anasogea pembeni kidogo, nami namfuata, anaweka beseni chini na kukaa katika kivuli kilichosababishwa na bango kubwa la tangazo la kampuni ya simu za mikononi.

Tukiwa wote tumekaa, ananiambia kuwa mbali na tabia yake ya kujituma kumfanya kuuza nazi na mihogo mibichi, ila hali ya mumewe imemsukuma zaidi awe hivyo.

Anasema ni mwezi wa sita huu mumewe hana kazi na kila anapotafuta kibarua anaambulia patupu. Dada wa watu anaongea kwa simanzi sana hata inanifanya nami nisawajike na sura.

Anazidi kueleza kuwa yeye ni msomi na ana shahada ya sayansi ya kompyuta ila amelazimika kuuza nazi barabarani baada ya kuhangaika kutafuta kazi na kukosa huku mumewe naye akipoteza kazi katika mazingira tatanishi.

“Kaka maisha yangu yamejaa utata sana. Japo nimetoka katika familia inayojiweza kwa kipato huku mimi mwenyewe nikiwa na elimu angalau ya kuweza kunisaidia katika maisha ila nimekuwa nikijikuta katika mitihani mizito sana.” Anatulia kidogo huku akiangalia chini akionekana kuhisi uchungu, anatoa leso na kujifuta machozi.

Ananipa mkasa wa kusisimua sana. Japo anatoka katika familia yenye uwezo ila familia yake imemtenga kwa sababu ya kuamua kuwa na mwanaume ambaye familia hiyo haijamtaka.

Anasema japo alitumia kila aina ya ushawishi kuiaminisha familia yake hasa baba na mama yake kuwa mwanaume huyo ingawa anatoka katika familia ya chini kiasi ila ndiye anampenda na anaona ndiye chaguo sahihi katika maisha yake, ila familia yake haikuonesha kutaka kuelewa.

Na baada ya yote walikubali kishingo upande aolewe. Baada ya hapo wakamtenga. Hawamjui katika shida wala katika raha. Kila anapohitaji msaada wa aina yoyote hawaoneshi kujali zaidi ya kumwambia maneno ya kejeli.

“Kaka yangu japo niko katika hali ngumu kwa sasa ila sitokata tamaa kwa sababu ni kweli nampenda sana mume wangu na siko tayari kumuacha. Najua haya yatapita, najua ipo siku tutapata thamani zote za kimaisha na kuendelea kufurahia maisha yetu.” Anamaliza kusema binti huyu anayeitwa Jackline.

Mapenzi ni pamoja na kuwa tayari kwa lolote kwa ajili ya mwenzako na kulinda penzi lako. Wewe unayeambiwa kuwa unapendwa na kujaliwa, je, ni kweli mpenzi wako yuko tayari kulipigania penzi hilo kwa kila namna? Je, marafiki zake ama ndugu wakionesha kutokukubali, yeye ataendelea kukung’ang’ania au basi itakuwa imetoka?

Napata mikasa mingi sana ya kimapenzi. Mingine inasumbua sana akili mpaka unasema ni kweli hawa walipendana!

Mara ngapi umewahi kusikia kuwa watu wameachana kisa marafiki zake wamesema hapendezi kuwa na mwanaume yule? Kama rafiki yako anaweza kuingia katika maamuzi yako na kukusukuma umuache kwa sababu ya kijinga kama hii, unasema vipi uliwahi kumpenda mwanaume yule?

Mapenzi si suala la kusema ‘babe I love you’. Mapenzi si suala la kushinda katika mitandao ya kijamii kutwa mna chati. Mapenzi ni suala nyeti linalohusisha maamuzi magumu na ya kujitoa muhanga.

Hata kama watu wote watasema kuwa hupendezi kuwa na msichana yule kisa sijui mfupi sana au hana elimu kama wewe, ila kama kweli unampenda kwa dhati hutojali hayo, utaendelea kuwa naye kwa upendo ule ule na tena hata kuwaona hao wanaojiita marafiki zako kuwa ni wapuuzi fulani hivi wanaofaa kupuuzwa.

Ni upotofu kuamini fulani alikupenda sana wakati alikuacha kisa wewe masikini. Ni ujuha kuwaza kuwa bila dada yake kuingilia katika mahusiano yenu, fulani angekuwa wako kwa sababu alikupenda sana.

Waliosema mapenzi ni upofu walikuwa na maana kubwa. Kama fulani anakupenda kweli. Kwa dhati na yakini ya nafsi yake, abadani asilani, hawezi kuona wenye mali wala kusikia maneno ya kina fulani kuwa aachane na wewe.

Mapenzi ya kweli hayana visababu sababu visivyo na msingi. Eti ‘ babe nakupenda sana, ila naomba tuachane kwa sababu marafiki zangu huwa wanasema hatuendani.’ Anayekwambia hivi fahamu hajawahi kugusika na hisia zako. Mapenzi ni kujitoa sadaka dhidi ya maneno ya watu na shida nyingine.

Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kusikia habari ya msichana mmoja mrembo aliyeamua kutoka kuishi na wazazi wake Mikocheni B na kwenda kuishi Keko Machungwa kwa mpenzi wake.

Japo binti yule alikuwa na elimu kubwa huku akiwa kalelewa katika mazingira ya kisasa sana, ila mapenzi yalimfanya ayaone mazingira ya kwao ‘Uzunguni’ sio salama sana kwa furaha yake kulinganishja na Keko Machungwa.

Kwa akili ya tamaa utasema huyo ni mjinga, ila kwa hisia za kweli za mapenzi utaona binti jinsi anavyosukumwa na mapenzi na kufanya maamuzi magumu ambayo bila hisia halisi za mapenzi hayawezekaniki. Huyu analeta maana kamili ya mtu kupenda kwa sababu kajitoa sadaka kwa ajili ya mpenzi wake.

Mpenzi wako yuko tayari kufanya jambo gani gumu kwa ajili ya kuonesha ni namna gani anakupenda? Ukiachishwa kazi ama kufilisika, ataendelea kukuita ‘babe’ na kukufanyia yote mazuri ya hadharani na sirini anayokufanyia sasa katika hali nzuri?
 
Thamani ya upendo haipimiki hasa kwa yule ajuae uzito wa pendo lenyewe.....Sio hii pendapenda ya mdomoni tu, kumbe moyoni hamna kitu
Anakua na wewe kwa malengo fulani
ama kupata kitu fulani ..vikiondoka ndo basi tena ..unaanza kutafutiwa sababu
 
Mapenzi ni mojawapo ya feelings.,, Feelings unaweza kuzitii, kutozitii au kuzidirect somewhere else...,!! ni ww utakavyoamua...!! Hufi wala hupati madhara ya kibaolojia usipozitii feelings zako.,, Binafsi ziendekezi mafeeling yasio nisaidia maishani and i choose to be rational and use Feelings in my own advantage..,,!!

Mfano kwenye swala la mapenzi binafsi ziwezi chukua Mtu ambaye hana economic future na maisha yake mwenyewe..,, "Nimemchagua ambaye nitampenda baadae" kwa kufupi but "cjamfeel pengine kwa wakati huo"...,, Wew unayeendekez mafeeling ndo mnakujaga kufa na mistress kibao na mi pressure juu yake.,, BE RATIONAL and don't be a slave to your own feelings which you can control them...!!

By the way African in our traditions toka zamani izo hatuna tamaduni za kuendekeza feelings za mapenzi.,, WE CHOOSE TO LOVE and WE NORMALLY DO NOT FEEL TO LOVE SM1....!!
 
Mapenzi ni mojawapo ya feelings.,, Feelings unaweza kuzitii, kutozitii au kuzidirect somewhere else...,!! ni ww utakavyoamua...!! Hufi wala hupati madhara ya kibaolojia usipozitii feelings zako.,, Binafsi ziendekezi mafeeling yasio nisaidia maishani and i choose to be rational and use Feelings in my own advantage..,,!!

Mfano kwenye swala la mapenzi binafsi ziwezi chukua Mtu ambaye hana economic future na maisha yake mwenyewe..,, "Nimemchagua ambaye nitampenda baadae" kwa kufupi but "cjamfeel pengine kwa wakati huo"...,, Wew unayeendekez mafeeling ndo mnakujaga kufa na mistress kibao na mi pressure juu yake.,, BE RATIONAL...!!

By the way African in our traditions toka zamani izo hatuna tamaduni za kuendekeza feelings za mapenzi.,, WE CHOOSE TO LOVE and WE NORMALLY DO NOT FEEL TO LOVE SM1....!!
Kuna mambo siwez kukubaliana na wewe na hayapo.hivo, ila humu jf kila mtu yupo free kutoa mawazo yake. Shukran kwa your own thoughts.
 
Back
Top Bottom