ItsMi
Member
- Sep 13, 2021
- 66
- 31
Ufanye vifuatavyo ambavyo ni baadhi ya njia, au mbinu na vitu vya kuzingatia unapotaka ufanye biashara.
1. Kwanza unahitajika kufanya tafiti katika upande wa masoko kwa bidhaa yako husika.
2. Mtaji wa biashara unayoenda kuanzisha kwa sababu kama tunavyojua huwezi kufanya biashara itakayokuletea mafanikio pasipo mtaji.
3. Pia ni lazime utafute nyaraka kwa ajili ya ulipaji kodi ikiwa ni pamoja na hatimiliki ya biashara, ambapo vyote hivyo vinapatikana katika mamlaka za mapato ya nchi yaani (TRA).
4. Unatakiwa kuzingatia pia ni mahali gani au eneo gani biashara hiyo utaiweka na kwa kuzingatia uhitaji wa bidhaa husika.
5. Miundombinu bora kwa usafirishaji wa bidhaa zako zinapokuwa zinatoka na kuingia mahali unapofanyia biashara
6. Pia ni lazima uwe na bidhaa au huduma itakayokuwa bora ili kuchochea Ushindani kwa biashara yako na watu wengine kwa sababu ushindani unasaidia kutofautisha kilicho bora na kisicho bora hii itasaidia kumvuta mteja anunue dukani kwako.
7. Ni lazima bidhaa zako ziwe na Ubora kwa sababu mteja hupenda bidhaa bora na uaminifu ili siku nyingine aweze kuja dukani kwako na kukuungisha tena.
8. Inakubidi kuwa na lugha nzuri kwa Wateja muda wote bila kuchagua wala kubagua.
9. Inatakiwa ujue hasara na Faida ya biashara unayofanya ili uweze kujua jinsi gani ya kujinusuru na kufirisika.
Asante.