Unapo gombea Uongozi ili uwaibie Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unapo gombea Uongozi ili uwaibie Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Jan 2, 2011.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikijaribu kutafakari historia ya uongozi wa tanzania Tokea wakati wa awamu ya kwanza mpaka hii ya Sasa.
  Kihistoria Mwalimu alichaguliwa na wenzake nae akajaribu kufanya aliyo weza ili kuwakomboa wa Tanzania.
  Mwinyi hakukimbilia uongozi lakini wenzie walimuona anafaa waka mchagua kutuongoza.
  Ben aliombwa na Mwalimu akapigiwa Debe dhidi ya wengineo waliojitokeza, ikiwemo Malecela, Boyz 2 men etc. akafanya aliyoweza na mapungufu yake.
  Jakaya mrisho wa Kikwete hakuombwa na wenzake au kiongozi Yoyote aliye pita Bali Yeye mwenyewe alijiona kwamba ndio anaye faa kuwaongoza watanzania, nao wakaitikia ombi lake kwa kumpa ushindi wa kishindo muhula wa kwanza, lakini bahati mbaya dalilili zinaonyesha kwamba alijitolea kuchukua nafasi kwa manufaa ya watu wengine ( Wafadhili wa kampeni yake badala ya Mamilioni ya watanzania walio mpaka kura)
  Sasa najiuliza Licha ya hao wanao gombea uraisi kuna hata wana ogombea ubunge , udiwani na kadhalika ambao wanafanya kinyume cha matarajio ya walio wachagua.
  hatu katai kila bina damu ana mapungufu yake, lakini kinacho gomba ni pale mtu anapokuwa amekwenda tofauti saaana na malengo yanayo tarajiwa na wapiga kura wake.
  hivyo ninapenda kujiuliza Je viongozi wetu wanagombea ili watuibie au ili kutukomboa na lindi la umasikini/uduni tulio nao katika nanja nyingi iwe elimu, nishati, afya, makazi na huduma nyinginezo.
   
Loading...