Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,420
Kuna watu wamenishangaza sana, wanakimbilia kuchukua mikopo benki ili wakanunue hisa. Najiuliza haya mawazo watu huwa wanayatoa wapi?
Wanayo tabia ya kujielimisha binafsi kabla ya kuchukua hatua?
Wanayo tabia ya kuomba ushauri kwa wenye uelewa kabla ya kufanya kitu?
Iko hivi rafiki, unapotaka kufanya kitu chochote ambacho hujawahi kufanya kwenye maisha yako, unahitaji ujielimishe na ukielewe kwanza kitu hicho kabla ya kuchukua hatua.
Na njia za kujielimisha zipo mbili kwa kuanzia;
1. Soma vitabu vitano bora kwenye kitu hicho.
2. Kaa chini na mtu mwenye uelewa wa jambo hilo na akushauri vizuri.
Sasa kama huna muda wa kujielimisha kabla ya kuchukua hatua, usilie pale unapofanya maamuzi ya hovyo.
Na hii ni kwa kila jambo, siyo hisa tu, iwe ni kufuga kuku, bata au hata nyuki. Iwe ni kuanza biashara au hata kuanza familia.
Jenga tabia ya kujielimisha kabla ya kufanya maamuzi.
Kocha Makirita,
www.amkamtanzania.com
www.kisimachamaarifa.co.tz