Unanilostisha tu bora niende zangu...............

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Yalikuwa maneno ya kipenzi changu kuanzia 1990 hadi 2004, vitoto vinakua , tukaona tutafute mbadala wa kipato badala ya kutegemea kamshahara kangu tu.tukaanzisha biashara, na msimamizi akawa ni yeye, mwenzangu huko akapata walimu wakampa somo likamkolea. nyumbani kukawa hakuna amani, hisani na maisha ya watoto hakuvijali akili yake ikawa kuvunja nyumba na kukimbilia utajiri ....., wazee wakatusuluhisha lkn sikio la kufa halisikii dawa. nyumba ikavunjika . tangu wakati huo hadi leo ni ndg zake tu ndo wanaokuja kuangalia watoto ,yeye ni aibu kwenda mbele. amejaribu namna turudiane uwezekano huo umekosekana kwani mimi tayari nimeoa , maisha yamempiga kisawasawa namuonea huruma lkn mchuma janga hula na wa kwao. nimejifunza jambo ktk maisha ya ndoa , usitupe penzi alilokupa MUNGU kwa kutaraji kupata kwa akili yako utachemka.
 
Huwa ni kawaida ya baadhi ya wanawake.Wakiwa na aina fulani ya maisha wanawakataa wenzi wao wa kitambo au hawawataki wanaume wa aina fulani!
 
Tunza wanao, make more money usithubutu kumrudisha huyo kiruka njia, atakurudisha nyuma sana.
 
ni kweli hutakiwi kutupa penzi..ila unaonaje ukimfanya kama kimada tu maana old is gold bwana uezi jua
 
Kwenye Imani yangu tunaamini kwamba riziki ya wote wanaokutegemea nyumbani kwako hupitishiwa kwako- na kama tujuavyo rizki tupewazo na mungu hazilingani, kila mtu anajaliwa kulingana na mapenzi yake. Inawezekana mume/mke akajaliwa kipato kikubwa kuliko mwenzie lakini kinapitia kwa anayetoka kwenda kutafuta, siku kila mmoja akienda njia yake huenda na rizki yake; ndio maana mara nyingi familia iliyo na maisha mazuri mmoja huadhirika pale wanapotengana.

My take-mng'ang'anie uliye naye kama una ridhika na hali uliyonayo.
 
Yalikuwa maneno ya kipenzi changu kuanzia 1990 hadi 2004, vitoto vinakua , tukaona tutafute mbadala wa kipato badala ya kutegemea kamshahara kangu tu.tukaanzisha biashara, na msimamizi akawa ni yeye, mwenzangu huko akapata walimu wakampa somo likamkolea. nyumbani kukawa hakuna amani, hisani na maisha ya watoto hakuvijali akili yake ikawa kuvunja nyumba na kukimbilia utajiri ....., wazee wakatusuluhisha lkn sikio la kufa halisikii dawa. nyumba ikavunjika . tangu wakati huo hadi leo ni ndg zake tu ndo wanaokuja kuangalia watoto ,yeye ni aibu kwenda mbele. amejaribu namna turudiane uwezekano huo umekosekana kwani mimi tayari nimeoa , maisha yamempiga kisawasawa namuonea huruma lkn mchuma janga hula na wa kwao. nimejifunza jambo ktk maisha ya ndoa , usitupe penzi alilokupa MUNGU kwa kutaraji kupata kwa akili yako utachemka.

Hayo ni matokeo ya kawaida! Kuna tunaoambiwa w a s e ng e baada ya kwishamzalisha mtu watoto wanne.
 
Huyo aliyekimbia nyumbani kwake bila kufukuzwa na kuishi mwenyewe nje kwa uhuru bila usimamizi wa mume hafugiki tena. Ukimchukua ni sawa tu na kujaribu kufuga kunguru kwani ataishia kukupasua kichwa tu. Busara ya kawaida inakutaka ukae naye mbali. Kama unamhurumia, kwa sababu ni mama wa watoto wako, na una uwezo basi msaidie mtaji aanze biashara nyingine kama ataweza.
 
Back
Top Bottom