Unamshauri nini huyu kijana?

Unamshauri nini huyu kijana?

Yofav

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
4,309
Reaction score
7,857
Ni kijana wa 24yrs old ana miaka 6 sasa hapa Dar es Salaam kumaanisha ameingia jiji hili akiwa 18yrs.

Ni kijana ambae anahisi alizaliwa kwa bahati mbaya kwamba ni kama wazazi wake hawakujipanga na ujio wake kutokana na aina ya maisha aliyokulia anahisi kuna vitu vingi amevikosa kutoka kwa wazazi wake, Picha inaanza wazazi wake walitengana muda mfupi tu baada ya kijana huyu kuzaliwa, Amekuwa kwa kulelewa na mzazi mmoja kwa kudangdang (Leo kwa mama kesho kwa baba) Mama yake akaolewa na mwanaume mwingine na akapata mtoto mwingine wa pili ambae ndo tuseme ni dada wa huyu kijana, Mama yake anaachika tena anapata mwanaume mwingine anazaa mtoto wa tatu na mwanaume mwingine anapata mtoto wa tatu wa kiume ambae tuseme ni kaka mtu wa huyu kijana (Wakati huu wote kijana analelewa na baba)… Yote ya yote bado mama wa kijana huyu anatelekezwa tena na huyo mwanaume wa tatu na sasa amekuwa single mother.

Elimu ya huyu kijana inasuasua kutokana na mzazi kukosa uwezo wa kumkomalia kimasomo akaishia upili kwa kukosa wa kumuendeleza na ndipo akaanza safari yake ya mtaani kutoka mkoa aliokuwa akilelewa na mzazi wake mmoja (baba) ambae ambae baada ya kijana kumaliza elimu ya upili kwake aliona kama ndo kashamalizana na kijana hivyo kijana aangalie ustaarabu wake… Baba anarudisha mpira kwa kipa kutokana na ugumu wa maisha anaenda kuishi kwa wazazi wake kijijini (Kwa bibi wa kijana)

Maisha ya kijiji yanamshinda kijana anaamua kuhama kijijini na kuja mjini (Dar) kujitafuta anamuacha baba kijiji X kwa wazazi wake na pia anamuacha Mama jiji X akiwa na watoto wawili huku baba zao wakiwa hawajulikani walipo (Lakini heri kwa mtoto wa pili kwa kuwa ndugu zake wana uwezo hivyo mtoto wa pili anakuwa na uhakika wa malezi bora kutokana na support ya ndugu wa upande wa baba yake)

Kijana anafika Dar anapambana kiasi cha kulizoea jiji na kuweza kujitegemea 100% na hivi sasa simu zimekuwa zikiingia za kuombwa misaada na hawa wazazi wake… Ubaya ni kwamba wazazi hawaoneshi kujali kijana anaishi vipi wala kujiahughulisha na nini bali wanachoona cha maana kwao ni miamala ikisoma kwa simu zao, Kijana anajitahidi kuwatimizia kwenye baadhi ya mambo madogo kwakuwa bado pia hajawa na uwezo wa misaada mikubwa ambayo asilimia kubwa ya wazazi huitegemea kwa watoto wao.

Issue inakuja kuwa kwamba upendo na kujali kwa mama wa kijana upo zaidi kwa wale madogo wawili, Mama anaonesha kuwazingatia sana wale watoto wengine kiasi inafanya kijana aone kwamba mbona yeye hakuoneshwa upendo ule, Mbona hao madogo wenzake wanapambaniwa sana kusoma, Imagine Dogo namba mbili katoka kuua six mwaka jana na hivi sasa anapambaniwa aende chuo na kinachomfanya huyu kijana ahisi maisha hayapo sawa kwake ni pale ambapo inafika muda mama mtu anapompigia simu kumtaka ampatie huduma mbalimbali dogo namba mbili ili asikwame, Mfano anaweza kupokea simu ya ombi la kumtaka amnunulie dogo namba mbili Simu,Pc n.k vya kumuwezesha kusoma na kuishi kisasa ilihali yeye alitelekezwa na hakuwahi kuzingatiwa kiasi hicho since alivyofika 17yrs ni kama alianza kujilea na kujitegemea kwenye kila kitu

Sasa imefika muda wazazi wa kijana huyu wanaona kama ni haki yao kijana kuwatatulia changamoto zao na ikiwa kijana anaonesha kusuasua kwa kudai hali haipo shwari basi wazazi hawa kila mmoja huanza humtuhumu kijana huyu kwamba itakuwa anapendelea upande mmoja, (Yaani mama uhisi kuwa kijana atakuwa anamsaidia baba pekee, Na baba pia uhisi kijana humpendelea sana mama)

Kijana yupo kwenye wakati mgumu kwa kuwa wakati mwingine anatamani hawa wazazi wangekuwa wakiishi pamoja walau akituma japo 30000/= inaweza kuonekana kubwa kwao kuwatatulia baadhi ya shida zao kwa pamoja lakini 30000/= hiyo humpasa kijana kuiganya mara mbili jambo ambalo anapoituma kwa kila mmoja wao basi wazazi wake hunung’unika kwamba kijana anatuma hela ndogo isiyotatua chochote.

Kijana huyu ni rafiki yangu, Mara nyingi ni mtu anaejiona kama looser/asie na bahati/asie na furaha ya kudumu katika maisha yake… Nipo na wazo la kumahauri ila kabla ya kumshauri ningeomba nione nanyi mna mawazo gani ili nisijekuwa nabomoa kumbe kuna wazo la busara ambalo linaweza kujenga kutoka kwenu
 
Kwa upande wangu hapo wa kumzingatia kidogo no baba, kwa sababu yeye alijitahidi kumsogeza kijana hadi kwenye upili. Alinyoosha mikono baada ya maji kuzidi kichwa na kuamua kurudi kijijini kwa wazazi.

Mama yupo kwa ajili ya kuchuma tu kupitia cheo cha uzazi wa mchongo.
 
Ni kijana wa 24yrs old ana miaka 6 sasa hapa Dar es Salaam kumaanisha ameingia jiji hili akiwa 18yrs.

Ni kijana ambae anahisi alizaliwa kwa bahati mbaya kwamba ni kama wazazi wake hawakujipanga na ujio wake kutokana na aina ya maisha aliyokulia anahisi kuna vitu...
Kwani jukumu la kusaidia wazazi ni la lazima au kujitolea tu
 
Kuna kipindi katika maisha ubinafsi ndio kitu pekee mwanadamu anapaswa kuwa nacho.

Mwambie dogo umri haurudi nyuma. Akiendekeza kutengeneza maisha ya wengine ya kwake yataharibika na mwisho wa siku maisha yake ya utotoni y kuwa na tabu yatajirudia tena uzeeni akiwa kapuku.

Hakupata familia aliyoitaka alipokuwa mtoto. Sasa ni wakati wa kutengeneza familia anayoitaka kwa kujijenga kimaisha na kuhakikisha anaweka misingi bora kwa watoto wake.

Kuweza kwake ku survive toka akiwa na miaka 17 ni ithibati tosha kuwa haitaji msaada wa yeyote baina ya hao wanaomnyonya. So ifike wakati awatenge ili yake yaende.
 
😁😁!

Wacha wampe mwongozo!
Sema ajifunze kusamarize sasa Maelezo mengi sana yanachosha
Hathaminiwi wala kupewa attention na wazazi...
Mama yake kazalishwa na wanaume tofuati tofauti...
 
Huyo kijana ni wewe Ila mwambie ajitahidi asimame yeye Kama yeye kwanza .

Akimaliza kusimama itakuwa rahisi kuwasimamisha wengine.

Kuhusu wazazi ajitahidi awaguse kwa njia chanya pasipo kuwaumiza au yeye kujiumiza.
 
Ni kijana wa 24yrs old ana miaka 6 sasa hapa Dar es Salaam kumaanisha ameingia jiji hili akiwa 18yrs.

Ni kijana ambae anahisi alizaliwa kwa bahati mbaya kwamba ni kama wazazi wake hawakujipanga na ujio wake kutokana na aina ya maisha aliyokulia anahisi kuna vitu vingi amevikosa kutoka kwa wazazi wake, Picha inaanza wazazi wake walitengana muda mfupi tu baada ya kijana huyu kuzaliwa, Amekuwa kwa kulelewa na mzazi mmoja kwa kudangdang (Leo kwa mama kesho kwa baba) Mama yake akaolewa na mwanaume mwingine na akapata mtoto mwingine wa pili ambae ndo tuseme ni dada wa huyu kijana, Mama yake anaachika tena anapata mwanaume mwingine anazaa mtoto wa tatu na mwanaume mwingine anapata mtoto wa tatu wa kiume ambae tuseme ni kaka mtu wa huyu kijana (Wakati huu wote kijana analelewa na baba)… Yote ya yote bado mama wa kijana huyu anatelekezwa tena na huyo mwanaume wa tatu na sasa amekuwa single mother.

Elimu ya huyu kijana inasuasua kutokana na mzazi kukosa uwezo wa kumkomalia kimasomo akaishia upili kwa kukosa wa kumuendeleza na ndipo akaanza safari yake ya mtaani kutoka mkoa aliokuwa akilelewa na mzazi wake mmoja (baba) ambae ambae baada ya kijana kumaliza elimu ya upili kwake aliona kama ndo kashamalizana na kijana hivyo kijana aangalie ustaarabu wake… Baba anarudisha mpira kwa kipa kutokana na ugumu wa maisha anaenda kuishi kwa wazazi wake kijijini (Kwa bibi wa kijana)

Maisha ya kijiji yanamshinda kijana anaamua kuhama kijijini na kuja mjini (Dar) kujitafuta anamuacha baba kijiji X kwa wazazi wake na pia anamuacha Mama jiji X akiwa na watoto wawili huku baba zao wakiwa hawajulikani walipo (Lakini heri kwa mtoto wa pili kwa kuwa ndugu zake wana uwezo hivyo mtoto wa pili anakuwa na uhakika wa malezi bora kutokana na support ya ndugu wa upande wa baba yake)

Kijana anafika Dar anapambana kiasi cha kulizoea jiji na kuweza kujitegemea 100% na hivi sasa simu zimekuwa zikiingia za kuombwa misaada na hawa wazazi wake… Ubaya ni kwamba wazazi hawaoneshi kujali kijana anaishi vipi wala kujiahughulisha na nini bali wanachoona cha maana kwao ni miamala ikisoma kwa simu zao, Kijana anajitahidi kuwatimizia kwenye baadhi ya mambo madogo kwakuwa bado pia hajawa na uwezo wa misaada mikubwa ambayo asilimia kubwa ya wazazi huitegemea kwa watoto wao.

Issue inakuja kuwa kwamba upendo na kujali kwa mama wa kijana upo zaidi kwa wale madogo wawili, Mama anaonesha kuwazingatia sana wale watoto wengine kiasi inafanya kijana aone kwamba mbona yeye hakuoneshwa upendo ule, Mbona hao madogo wenzake wanapambaniwa sana kusoma, Imagine Dogo namba mbili katoka kuua six mwaka jana na hivi sasa anapambaniwa aende chuo na kinachomfanya huyu kijana ahisi maisha hayapo sawa kwake ni pale ambapo inafika muda mama mtu anapompigia simu kumtaka ampatie huduma mbalimbali dogo namba mbili ili asikwame, Mfano anaweza kupokea simu ya ombi la kumtaka amnunulie dogo namba mbili Simu,Pc n.k vya kumuwezesha kusoma na kuishi kisasa ilihali yeye alitelekezwa na hakuwahi kuzingatiwa kiasi hicho since alivyofika 17yrs ni kama alianza kujilea na kujitegemea kwenye kila kitu

Sasa imefika muda wazazi wa kijana huyu wanaona kama ni haki yao kijana kuwatatulia changamoto zao na ikiwa kijana anaonesha kusuasua kwa kudai hali haipo shwari basi wazazi hawa kila mmoja huanza humtuhumu kijana huyu kwamba itakuwa anapendelea upande mmoja, (Yaani mama uhisi kuwa kijana atakuwa anamsaidia baba pekee, Na baba pia uhisi kijana humpendelea sana mama)

Kijana yupo kwenye wakati mgumu kwa kuwa wakati mwingine anatamani hawa wazazi wangekuwa wakiishi pamoja walau akituma japo 30000/= inaweza kuonekana kubwa kwao kuwatatulia baadhi ya shida zao kwa pamoja lakini 30000/= hiyo humpasa kijana kuiganya mara mbili jambo ambalo anapoituma kwa kila mmoja wao basi wazazi wake hunung’unika kwamba kijana anatuma hela ndogo isiyotatua chochote.

Kijana huyu ni rafiki yangu, Mara nyingi ni mtu anaejiona kama looser/asie na bahati/asie na furaha ya kudumu katika maisha yake… Nipo na wazo la kumahauri ila kabla ya kumshauri ningeomba nione nanyi mna mawazo gani ili nisijekuwa nabomoa kumbe kuna wazo la busara ambalo linaweza kujenga kutoka kwenu
Katika imani yetu tunaambiwa kuwa "ukitaka haki zako basi wajibika".
Hao wazazi hawakuwajibika ipasavyo ila wanadai haki kwa kijana.
Ila yote ya yote ni wazazi,chamsingi awe na roho ya kupuuza asiwe mwenye kuzingatia ya wazee wake pale wanapomlalamikia.
Pia akunjue tu nafsi,ila suala la kusaidia hao wadogo zake sio la lazima kwake na wala asijitwishe mzigo kiulazima hivyo.
Akiweza asaidie akishindwa atulie na wala asinung'unike.
Maana ndugu wenyewe hawaeleweki,unakuta uhamuhangaikia mtu ila hatokuja kukumbuka kama uliwahi kumhangaikia.

Neno la kuzingatia awasaidie tu wazazi wake kwasababu ni wazazi,ila akikwama asijilazimishe.
Na hao wadogo zake HAKUNA ULAZIMA WA KUWASAIDIA.
Ajikite kujenga maisha yake sio kuhangaika na ya wengine.
 
Unaweza kujitutumua unatoa ushauri kumbe ni tangawizi iliyokolea
 
Back
Top Bottom