Mara kwa mara nimekutana na komment za watu mbalimbali wakidharau neno la Mungu kwa kigezo kwamba Mungu kama yupo kwanini hakujibu maombi yao?
Watu hao wengi wao waliwai kuwa watoto wa Mungu na waliwai kushuhudia nguvu za Mungu lakini kutokana na changamoto za hapa na pale wamejikuta wakidharau nguvu za Mungu.
Watu awa pamoja na kushuhudia nguvu za Mungu na matendo yake makuu mara kwa mara la kini Mungu aliposhindwa kujibu haja ya moyo wao wamekasirika na kumwoma Mungu sio kitu.
Nataka nikuulize swali kama unafanya kazi sehemu yoyote ulishawai kumwomba jambo lolote bosi wako akakufanyia mambo yote? Yaani kila hitaji lako bosi wako alitekeleza kama ulivyo omba?
Wewe ni Mke au Mume kuna maombi ambayo ulifanya kwa mumewe au mkewe akakufanyia? Maombi yako kwa mke/mumewe uwa yanafanyika kama unavyoomba?
Unamlinganisha Mungu na Nani? Unadhania Mungu ni kifaa au kinyago ambacho unaweza kukiambia fanya hivi kikafanya? Au ukakielez chochote kikafanya?
Wale wanaokwenda kwa waganga wanajua ukuu wa miungu yao ndio maana wanapokwenda lazima kwanza watekeleze maelekezo ya miungu yao ili waweze kupata ushindi.
Una jua amri za Mungu? Unazifanya zote? Ayubu alipojua kwamba Mungu ni Mkuu alinyenyekea
Mungu ni muumba wa Mbingu na Nchi, kama leo hii ukikutana na kiongozi wa serikali unaweza kupiga magoti au kusalimia kwa heshima zote unafikiria Mungu ni mdogo kuliko viongozi wa serikali?
Kama leo hii unapotaka jambo lako lifanyike unamwomba kiongozi wa serikali na anakuhaidi lakini anaweza kufanya au kutokufanya na hauna uwezo wa kumfanya chochote
Mungu ni mfalme Mkuu, ni Mfalme wa Wafalme , Mungu Mwenye Nguvu, Mungu Mwenye Enzi, unamlinganisha na Nani.
Ile Mungu hajakujibu kama unavyotaka ujue amekupenda, Ibrahimu aliomba kupata mtoto miaka 25.
Umeombea jambo moja tu mwaka unaona umeomba kweli unafikia hata ujasiri wa kumkashifu Mungu
Yusufu alikaa miaka 17 kabla ya kuwa waziri Mkuu, na hakuwai kulalamika mbele za Mungu
Daudi alikaa miaka 13 kabla ya kuwa mfalme lakini hakuwai kutoa maneno juu ya Mungu
Wewe ni nani hata umseme Mungu vibaya?