Unambeep mtu, akikigia hupokei, Inakera sana

Mgirik

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
13,208
13,233
Kuna haya mambo tunayoyafanya-
. Unambip mtu akikupigia hupokei
. Unabip ukipigiwa unajibu nilikuwa nakusalimia tu.
. Unaonana na rafki yako unamlaumu kuwa hakupigii simu ilhali hata ww unayo namba yake na hujawahi kumpigia,
. Umetongozwa umetoa mzigo umewekwa blacklist unaanza kulaumu kuwa amekuchezea na amechezea hisia zako wakat hamkukubaliana kuoana,
. Umeombwa namba ya simu tayar unaanza kupiga mzinga,
. Soksi zinanuka unakaribishwa kwa rafk au ndg unavua viatu nyumba nzima kama panya kaozea.
. Unamkuta mwenzako hotel au mgahawan anakula unaanza kumsemesha semesha.
. Kujifanya unajua kila kitu, kila maada inayoanzishwa ww unajifanya unaijua na unataka uisimulie ww tu.
. Kuombaomba bia bar wakat umejipeleka mwenyew.
. Kuelezea matatizo yako wakati kila mtu anayake,
. Kulazimisha kumpa mtu kadi ya harusi na kumnunia asipokuchangia wakat hayo umejitakia mwenyewe.

Yapo mengi endeleeni kuyaweka
 
Hiyo ya kuomba Omba bia naomba tusiwanyanyapae hao wadau tafadhali. Mimi kitambo wakati nasoma high school na Chuo nilikuwa naomba bia kwa kaka zangu nikiwa na kiu. Nina hakika hata wewe ulipitia au umeshawahi kuomba bia.
 
Back
Top Bottom