TLC waligunduliwa na Peebles ambaye ni mke wa producer maarufu Antonio L.A Reid. Reid akawasainisha kwenye lebo ya Laface ambayo ilikuwa ni ubia wa Reid na super-producer mwingine Kenneth "Babyface" Edmonds. Albamu yao ya kwanza ilikuwa ni "Oooh...On The TLC Tip" (1994) ambayo ilikuwa na hit singles kama "ain't 2 proud 2 beg", "what about your friends" na "baby baby Baby".
Albamu yao ya pili, "Crazysexycool" (1996)ndio iliwapandisha chati sana kupitia nyimbo zilizo-hit sana za "creep", "red light special", "waterfalls" na "digging on you". Mwaka 2000 walitoa "Fanmail" iliyokuwa na wimbo maarufu sana wa "no scrub".
Baada ya hapo mwaka 2001 walianza rekodi albamu yao ya nne inayoitwa "3D". wakiwa katikati ya kutengeneza "3D" Lisa "Left Eye alifariki kwa ajali ya gari huko Honduras. T-Boz na Chilli waliamua kumalizia albamu hiyo na kuitoa mwaka 2004. "3D" haikufanya vizuri sana na baada ya kufanya Tour ya kuipromoti Chilli na T-Boz waliamua kupumzika kurekodi ingawa wamekuwa wakitumbuiza kwenye matamasha mbalimbali.