Unakumbuka nini Siku kama leo Mtihani wa kwanza FM6?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Leo wadogo zetu wameanza rasmi mtihani wao wa kidato cha Sita, nawatakia kila la kheri...

Baadhi yetu humu tumepitia huko, je ni nini unakikumbuka siku kama hii?

Mimi nakumbuka Tulipata Gaka tukasolve weeee asubuhi mzigo unaingia Sio....

Nachokumbuka jamaa yangu pembeni ile anafungua tuu kuona sio akashindwa kujizuia..
Alisikika akisema

"Aaaiiiiiiiiiiiiii....." huku kashika kichwa,
Mwingne alitukana "Huu ni U...nge",
Msimamizi alisikika tuu akisema mkomee...

Hapa sasa ndio kila yule akaanza kufa kivyake...
Dk za mwanzo watu walikua hawatulii, full jasho lakini pia kulikua na momment za furaha kila yule akimuangalia mwenzake anavyosota basi ni kucheka bila kupenda, kalamu hazishikiki...

Mwisho wa siku wanaume wakatoboa maisha yakapita leo hii Tupo kwenye mtihani wa Maisha ambao hauna gaka...
 
😂😂😂😂

"Mkomeeee"
 
Nakumbuka jamaa yangu aliongeza booklet kwenye pepa ya GS chakushangaza yy peke yake ndo alipata F GS akapigwa Technical Division yaani 3.Niliwaza sana aliingia chaka kivipi.Mungu ni mwema asoma Bedcom sasa mwalimu wa Commerce
 
Wengine tuliyapata hayo magaka na tukaliwa vichwa.
Akili huna huna tu hata ukiwa mlinzi wa mitihani unayofanya kesho yake maana kuna wengine wanalala saa mbili siku ya pepa wanaamka muda wa kutoka parade na miezi michache baadaye anakuwa MUHAS au UD kwenye makozi mazitomazito.
 
Daaah, Mimi nakumbuka Sikh tunafanya Biology 1 / tulipewa possible fake , huku tulinunua kwa kuuza Matranka , very sad.

Hasira zote nimezimalizia kuwa mwalimu wa Elementary nakutembeza viboko.
 
Ilikua BAM, ile niliitoa kafara maana nili itumia kusoma upepo, lakini pia nilikua siisomagi..

Kesho yake PHY 1, Unakaribishwa na Errors ili kutolewa wenge, Halafu unaitwa kwenye Mechanics ikitawaliwa na Projectile, SHM, Fluid, Circular motion, hujatulia Current na Heat vinakusalimia..
Wenge lilikata lenyewe, hakuna siku nilishuhudia kalamu zikigoma darasani kama ile sikuu, Kamasi, jasho navyo vililindima, Tunatoka pale wale ma comedian wa darasa Ukituangalia nyuso zimeshuka kama Andazi liliofeli kuumuka..

Mwisho wa siku paper 11 zikawekwa kibindoni, wingi wa paper unakusaidi ku equalize pale ulipopotea, finaly tukatoboa...

Sasa Tuko upande wa pili ambao, Unajiuliza kwa nini niliteseka vile? ndio ulichokipata kina kusaidia ila sio kwa Jasho lilee...
Ningepata wa kunishauri kipindi kile Nilikua na shortcut nzuri sana kuliko kupitia advance..

Mwanangu Nikiona ana akili ya wastani, Advance haendiii, hasa comb niliyosoma mimi, ni kumtesa nakati kuna njia nyingi tuu za kutoboa maisha....
 
Nakumbuka hii siku vizuri sana, GS ilienda vizuri tuu paper 1 ya mathematics sikuona swali la kukosa kabisa, Paper 2 ilipokuja section B yote nilikua najua lakini ajabu nilipanik na kuanza kuhema,
Practical ya Chemistry nilipaliwa na Gas nikakimbizwa Zahanati pale Azania,
Anyway Mungu ni mwema siku zote, wadogo zetu kila la kheri
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kuna mmasai mmoja alipata umaarufu wa ghafla, nskumbuka tulikuwa kwenye practical ya physics jamaa pepa ilikuwa ngumu sana (Luna practical inaitwa boiler ilimshinda na swali lingine la potentiometer halo likamshinda akawa amebakiza swali moja tu)

Ghafla tukasikia tatataaaaaaaa kriiiii (jamaa alichana shati kama wacheza mieleka),

Ule mtihani ulikuwa mgumu sana, binafsi nilitoa kafara swali moja nkakomaa na mawili kwa kushusha full detail.
Mwisho wa siku nilitoboa
 
Leo wadogo zetu wameanza rasmi mtihani wao wa kidato cha Sita, nawatakia kila la kheri...

Baadhi yetu humu tumepitia huko, je ni nini unakikumbuka siku kama hii?

Mimi nakumbuka Tulipata Gaka tukasolve weeee asubuhi mzigo unaingia Sio....

Nachokumbuka jamaa yangu pembeni ile anafungua tuu kuona sio akashindwa kujizuia..
Alisikika akisema

"Aaaiiiiiiiiiiiiii....." huku kashika kichwa,
Mwingne alitukana "Huu ni U...nge",
Msimamizi alisikika tuu akisema mkomee...

Hapa sasa ndio kila yule akaanza kufa kivyake...
Dk za mwanzo watu walikua hawatulii, full jasho lakini pia kulikua na momment za furaha kila yule akimuangalia mwenzake anavyosota basi ni kucheka bila kupenda, kalamu hazishikiki...

Mwisho wa siku wanaume wakatoboa maisha yakapita leo hii Tupo kwenye mtihani wa Maisha ambao hauna gaka...
Nakumbuka nilitoka na point zote 3 muhimu
Gs & Bam
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom