Msamiati
R I P
- Mar 6, 2011
- 1,063
- 700
Kitu pekee kilichokuwezesha kufika hatua uliyopo kwenye mahusiano yako ni matarajio makubwa uliyokuwa nayo juu ya mapenzi yenu.
Kitu pekee kilichokufanya ukafika hatua uliyopo kwenye biashara yako, ni matarajio makubwa uliyo nayo juu ya hiyo biashara.
Kitu pekee kilichokufanya uingie kwenye mtanange wa kupigania malengo yako ni picha kubwa za matokeo yaushindi.
Uliona kuwa siku moja mwenzi ulie nae atakuwa baba au mama watoto bora kwenye familia yako, uliona kuwa yeye anaweza kuwa nguzo imara kwenye mapenzi na malezi ya familia yenu. Matarajio makubwa ya kupata mafanikio kwenye shuguri unayoifanya, kuwa mfanya biashara mashuhuri au kuwa msanii hodari anayejulikana kimataifa hicho ndicho kitu pekee kilichokupa nguvu yakufika hapo ulipo
Lakini sasa unaona hali imekuwa tete, Sasa unahisi hukufanya maamuzi sahihi, unaona hukufikiri vizuri kabla ya kuamua, unahisi huna elimu ya kutosha, unaona huna sapoti ya kutosha, huna msaada, huna ulinzi, huna watu waaminifu, huna mwangalizi, unaona huwezi kuwa na muda wa kutosha.
Umegundua kuwa kuimba si kipaji chako unajisumbua bure, sasaunatambua kuwa hujazaliwa kuwa mwanamitindo, unawaza kuwa biashara zinawenyewe wewe ni kama ulivamia tu.
Sasa unakubaliana na ukweli kuwa hukuumbwa kwa ajili yake ndio maana migogoro haiishi. Unaona maji yamekufika shingoni na huna njia m'badala kwa sasa zaidi ya kukata tamaa na kusitisha zoezi.
Katika maneno haya machache, ningependa usome simulizi hii fupi ikusaidie kufikia uamuzi wa mwisho.
Mwaka 1923 wanajiolojia wawili mmoja kutoka India na mwingine kutoka ufaransa walipata ramani ya eneo lililosemekana kuwa na hazina kubwa ya madini ya Dhahabu katikati ya Kenya na Tanzania.
Wanajiolojia hao walikubaliana kwenda kuchimba ili kuthibitisha, hivyo wakaamua kugawana maeneo, Mhindi akachimbe kutokea Tanzania na Mfaransa akachimbe kutokea Kenya.
Mtaalamu wa kupima umbali aliwaambia kuwa kuchimba mpaka eneo linalokisiwa kuwa na Dhahabu ni Km 10 kamau kichimba kutokea Tanzania na Km 15 kama ukichimba kutokea Kenya.
Mhindi alichagua kwenda Kenya na Mfaransa akaamua kuchimba kutokea Tanzania.
Kutokea kenya mhindi alichimba mpaka alipofikia km 10 alizoambiwa na mtaalamu lakini hakufanikiwa kupata chochote, mtaalamu alikuwa kapima vibaya badala ya kupata km10.1 yeye akapata km10 kamili. Mhindi akaamua kukusanya vifaa vyake na kurudi India.
Mfaransa alichimba mpaka km 12 bila dalili yoyote ya kukutana na dhahabu, alichoka sana na kukata tamaa. Aliishiwa na maji na chakula kilibaki kidogo, alipoelekea km 13 hewa ilikuwa nzito na udongo ulizidi kuwa mgumu.
Mfaransa aliamua kuchimbampaka amalize km 15 alizoambiwa na mpima umbali. Baada ya kumaliza km15 kama ilivyokuwa kwa Mhindi na yeye pia hakuona chochote, lakini kabla hajaamua kukata tamaa aliamua kumalizia kwa kuchimba tena futi1, hakuamini kuona lundo la dhahabu mbele yake. Mwisho
I write this from my own experience and is what I know, amini usiamini "mzigo siku zote huwa mzitomwisho wa safari" Hata ukibeba mzigo wa maembe kutoka morogoro kwenda kariakoo sokoni ukifika ubungo ndio utaona mzigo wako umeongezeka uzito mara dufu.
Hapo ndio utaona umebeba mzigo usiokuwa saizi yako, hapo ndio utaona kiu, hapo ndio utajikuta mpweke, utaona njaa hapo ndio utautua na kughairi safari.
Mhindi alipoona ameshapoteza nguvu nyingi na malengo yake hayatimii halafu muda unazidi kwenda, akaamua kuachana na shughuri ya uchimbaji, ilikuwa bado point moja tu afikie hazina ya dhahabu, lakini kukata tamaa kukamfanya arudi nyuma.
"Kabla ya kukata tamaa nakushauri ujiulize kwanini ulianza" Tafakari vizuri matarajio makubwa uliyokuwanayo wakati unaanza kisha fikiria nini kinastahili kukufanya usifikie malengo yako. Sababu ndogo ndogo zisikufanye ukashindwa kumalizia point moja iliyobaki, iambie nafsi yako kwamba, "it's notover until I win" .
Tambua kuwa vikwazo na ugumu haukosekani kwenye jambo lolote lenye manufaa makubwa, manufaa makubwa yote unayoyaona duniani ni matokeo ya uvumilivu na kutokata tamaa,
mara nyingi nimejifunza kwa Thomas Edison Mgunduziwa taa za balbu, jamaa alipigwa na shoti zaidi ya mara 80 bila kukatatamaa, mwisho akafanikiwa kupata kile kilichokuwa kwenye matarajioyake na hatimae jina lake limeingia kwenye vitabu vya kumbukumbu.
Ili uweze kufikia malengo yoyote makubwa, ili uwe msomi mzuri, ili uwe na mahusiano bora na ya kuigwa, ili uwe mfanya biashara maarufu, ili uwe msanii mashuhuri hii ndio kanuni kubwa ya mafanikio, visababu vidogovidogo visikufanye ukate tamaa.
Napolion Hill kwenye kitabu chake kinachoitwa think and grow rich alisema "A winner never Quit, Aquitter never win"
Hakunakukata tamaa shikilia mpini mpaka mwisho.
Jioni njema.