Unajuwa matumizi yake?

Nakumbuka niliinunua ili nikaibe game kule computer room ya shule. Kuna game zuri linaitwa "pit fall" lilikuwa na MB 94 na hii floppy ilikuwa inabeba MB 5 (sikumbuki vizuri)
 
Sijabahatika kutumia floppy disk kwa kuchezea game.
Ila nilikuwa na TV game ya ATARI pamoja na game stick yake. Lakini game niliyopenda zaidi ilikuwa Nintendo donkeykong.

Nakumbuka floppy disk ilivyonitesa chuoni. Ikirowa maji kidogo au ikitingishika, file inakwama kufunguka. Zile film ndani zilikuwa sensitive sana.



Nintendo Donkey Kong



ATARI TV game with joysticks
 
Bila floppy disc huiingii computer room!!

Hadi to ticha wa computer aliitwa flopy disc!!
 
Nakumbuka niliinunua ili nikaibe game kule computer room ya shule. Kuna game zuri linaitwa "pit fall" lilikuwa na MB 94 na hii floppy ilikuwa inabeba MB 5 (sikumbuki vizuri)
mkuu floppy ni mb 1.3 hivi...text only
 
Nakumbuka enzi hizo niliiokota kwenye majalala ya wazungu hata nilikua sijui ni kitu gani, nikaenda nayo shule nikawa nawadanganya wanafunzi wenzangu ni kamera, nawapanga wanaweka pozi la kuwapika picha, navuta kile kimfuniko cha bati na kukiachia kikifyatuka wanasubiria picha. Nilipokuja kujua hizo floppy na matumizi yake nilicheka sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…