Unajua maana na sababu za ugumba?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Tatizo la kutopata ujauzito 'Ugumba' (Infertility) hili tatizo lipo kwa mwanaume na mwanamke. Ugumba ni kwamba watu wawili mke na mume wanatafuta mtoto kwa mwaka mzima bila mafanikio.

Sababu za tatizo la ugumba ni pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume. Sababu za ugumba kwa mwanaume ni kama zifuatazo:-

Matatizo kwenye mbegu za uzazi
Kutoa kiasi kidogo cha mbegu za uzazi
Uwezo mdogo wa kujongea kwa mbegu, hali inayopelekea mbegu kushindwa kufikia yai la uzazi

Matatizo haya ya mbegu za uzazi kwa ujumla husababishwa na vitu vifuatavyo:-

Maambukizi kwenye Korodani au saratani

Korodani kupatwa na joto jingi, hali inayoweza kusababishwa na matumizi ya Sauna, kuvaa nguo za kubana sana pamoja na kufanya kazi kwenye mazingira yenye joto kali

Matatizo kwenye utoaji wa shahawa, ikiwa mirija ya kutolea shahawa imeziba basi zitashindwa kutoka nje na kuishia kwenye kibofu

Utumiaji wa dawa za kulevya
Umri, hii nayo ni sababu mojawapo kwakua uwezo wa kuzalisha kwa wanaume huanza kushuka katika umri wa miaka 40
Uzito uliokithiri
Msongo wa mawazo, hii hupunguza ufanisi kwenye tendo la ndoa

Kwa wanawake sababu za ugumba ni kama zifuatazo:-

Uvutaji wa sigara
Matumizi ya pombe
Uzito uliokithiri
Magonjwa yanayoambukizwa kwa ngono, hii hupelekea kuziba kwa mirija ya Falopia
Matatizo ya ulaji
Umri, kwa wanawake uzalishaji hushuka katika umri wa miaka 32
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom