Unajivunia nini kwenye chama chenu kwa sasa!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
wakuu, salaam,
Ndugu zangu, kuna kautafiti nafanya.Naomba kama wewe ni mwanachama wa chama chochote cha siasa usiye na maslahi ya moja kwa moja [si kiongozi na husukumwi na kusaka vyeo], unisaidie maswali yafuatayo;
1. Uko chama gani?
2.Unalipia kadi yako kila wakati bila kushinikizwa?
3.Bado unayofuraha na unajivunia kuwa ndani ya chama? au upo tuu kwa kuwa huoni pa kwenda! [usiogope kwa kuwa unatumia fake ID]
4.Ni kitu gani hasa (objectively) unajivunia kwa sasa ndani ya chama chako?

Natanguliza shukurani kwa wote watakaotoa 'useful info' kwa kujibu maswali ya Msingi.
Asante!
 
JF Ina majukwaa mengi, tafuta litalokufaa hii la siasa, hata huyo zitto na mkubo walishahama
 
nipo chadema
nimeahirisha kulipia kadi yangu
ndiyo. najivunia kuwa ndani ya chama
siri kubwa ya majivuno ni ubaguzi. we are superior than other Tanzanians within our part.
 
Najivunia na kuonesha kifuwa changu kilivyo maridadi na kuwa mwanachama wa ACT
Mzalendo halisi
 
JF Ina majukwaa mengi, tafuta litalokufaa hii la siasa, hata huyo zitto na mkubo walishahama

Ndugu. unaweza kunifahamisha kwamba zitto kaingia je humu?
Haudhani kuwa kama huna la kuchangia, ni bora tu ungepita kimya kama wenzako!?
 
Najivunia rangi ya njano, kwa sababu ndiyo rangi iliyovaliwa kwa juu na timu ya Taifa ya Brazil.
Si ulicheki gemu mkuu?
 
Chama changu ni Tanzania na nalipia kadi kwa kushiriki ujenzi wa taifa langu la Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii.
 
Ndugu. unaweza kunifahamisha kwamba zitto kaingia je humu?
Haudhani kuwa kama huna la kuchangia, ni bora tu ungepita kimya kama wenzako!?

Mada yenyewe ndiyo inapelekea michango iwe hivyo. tunaulizana mambo ya vyama humu, ili iweje? chama cha nini? leteni mada za kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa letu siyo siasa za kuulizana wewe chama gani. Haya mimi nina kadi ya DAR YONG AFRICAN, wewe je?
 
Ukiwa chadema ukifa utaiona pepo.
Lakini ukiwa c.c.m ukifa ni moja kwa moja jehanam.
C.c.
Mwanadiwani.
 
Hata mleta thread unaonekana unadalili za mtikisiko wa ubongo,maana siamini kama hujui kuwa masojaz wote na baadhi ya uwt ni wana chadema.
 
Huu utafiti wako ni kwa maslahi ya nani na umetumwa na nani ? Who are the beneficiaries ? ........
 
Nakushauri hiyo dhana ya kwamba mtu hawezi akafanya kitu chochote cha maana mpaka awe ametumwa, ni bora ukajilazimisha kuachana nayo, vinginevyo utaishi katika lindi la utumwa wa kifikra mpaka hapo utakapoamua kuufungua ubongo wako.
 
Hivi unafanya utafiti ambao final product haina mlaji and then ukiulizwa unawehuka ........who are the beneficiaries of your research ? This is a straight question .......Acha blah blah .......
 
Back
Top Bottom