boniuso
JF-Expert Member
- Mar 13, 2013
- 950
- 1,341
UNAJISIKIA NAMNA UNAVYOJIFIKIIRIA MUDA MWINGI
Duniani watu wengi hawana furaha kwa 80% kwa sababu wengi hawafikirii bali ni "reactive" badala ya "proactive"
Watu wachache sana takriban 10% ndiyo wenye tabia ya kuwa "proactive" ambapo unaposema proactive ni watu wenye kufikiri kabla ya kutenda na kujiandaa kukabiliana na tukio kabla halijatokea
Wengi ni reactive kwa maana husubiri jambo litokee kisha watafute wa kumlaumu.
Asilimia kubwa sana ya taarifa unazosoma, kusikiliza, kutazama kwa siku ni hasi kwa 80%
Vyombo vya habari huwa vinaripoti taarifa hasi nyingi kuliko chanya,watu huongea vitu hasi kuliko chanya
Ulifanyika utafiti mwaka 1998 nchini Marekani katika tafiti za saikolojia kulikuwa na uwiano wa 17-1
Yaani taarifa mbaya 17 huku nzuri ni 1
Huwa unapokea taarifa mbaya kila wakati za watu wenye tabia mbaya sana,matukio mabaya kama vile magonjwa kama ukimwi, Corona, malaria
Vifo,ajali, milipuko ya mabomu, mauaji,utekaji,rushwa, migogoro ya watu, uhalifu, ubadhirifu n.k
Utapokea taarifa hasi nyingi sana kuliko nzuri mfano mapigano ya Congo, vita Syria, Boko Haram, corona, wanasiasa kukwaruzana kwenye mijadala, uongozi mbaya, wivi, ujambazi, watu kujiua n.k
Kwa ujumla taarifa hizi hufanya akili iwe inaona mabaya kwa watu na kwa kila kitu kisha watu wakiwa na mtazamo hasi juu ya maisha utawalaumu?
Utalaumu mtu vipi kwa tabia zake mbaya wakati muda wote anapokea taarifa mbaya kuhusu watu wengine?
Kama.unasikia mabaya ya watu muda wote unawezaje kuwapenda?
Unapata hasira sio kwa sababu ya matukio bali fikra zako hasi za muda mrefu.
Kila taarifa unayopokea kila siku kila saa inakuwa na athari katika furaha yako na maisha yako
Kati ya mazuri ambayo watu wamefanya au mabaya ni taarifa gani unapokea sana kwa siku?
Mara ngapi umesikia matajiri hupata pesa kwa njia haramu na ili uweze kuwa na pesa kwa njia halali huwezi kutoboa swali utawezaje kuwapenda hao matajiri?
Unawezaje kumpenda mtu wakati unasikia mabaya yake tu muda wote?
Ukiwa hufikirii unapokea kila kinachokuja utakuwa mwingi wa lawama kupita kiasi
Umewekewa programu kichwani hivyo unatenda kama ulivyoandaliwa
Watu wengi watakukatisha tamaa wala sio kosa lao kwa sababu hawajazoea kuwapa watu matumaini
Watu watakusema kwa mabaya sio kwa sababu wewe ni mbaya bali wao wamezoea kusema mabaya muda mwingi
Watu hawatashukuru kwa msaada uanowapa sio kwa sababu msaada wako ni mdogo au hauna thamani bali hawana mazoea ya kushukuru wakifanyiwa mazuri.
Elewa watu vile walivyo sio vile unavyowaona.
Mtu kukuonyesha tabasamu sio kwamba wewe ni mzuri sana au special bali anakuwa mwenye furaha wakati huo.
Kama huamini kaa nae uone kama atakuonyesha tabasamu kila siku kila saa
Hawezi kufanya hivyo kwa sababu hisia zake zinabadilika hivyo na tabia yake hubadilika
Mtu akiwa na huzuni hawezi kuona uzuri wako
Mtu mwenye hasira hawezi kukusema kwa mazuri
Mtu mwenye wivu hawezi kukupa pongezi
Mtu mwenye chuki hawezi kukuonyesha upendo
Mtu asiesamehe makosa yake ya zamani hawezi kukusamehe wewe kwa makosa yako
Mtu ambaye hajipendi hawezi kukupenda atawezaje kukupenda wakati hajipendi yeye mwenyewe
Huwezi kumpa mtu kitu ambacho wewe mwenyewe huna
Unawezaje kumuonyesha mwenzio moyo wa huruma wakati hujawahi kujihurumia mwenyewe

Ukimuelewa mtu hawezi kukusumbua
Hakuna mtu ambaye anafurahia muonekano wake kwa 100% hayupo na hawezi kutokea
Kila mtu huona kuna sehemu akiifanyia maboresho atakuwa na mvuto sana
Watu hufikiria kuwa wakiwa hawana matatizo ndio watakuwa na furaha labda nikwambie ukweli hakuna binadamu duniani ambaye hana matatizo
Hata ambao unawaona wanacheka muda wote hawana furaha muda wote
Wewe mwenyewe huwezi kuanzia asubuhi mpaka usiku ukiwa unacheka tu haiwezekani
Lazima baadhi ya nyakati uwe na furaha kisha hasira zinakuja na hujui zimetoka wapi kisha akili itakaa bila furaha au huzuni kisha furaha inakuja na kuondoka mpaka siku inaisha
Ukisema huna tatizo hata moja utakuwa ndio tatizo lenyewe kuliko yote duniani
Hakuna mtu ambaye pesa kwake imetosha, afya, biashara, mahusiano vyote kuwa vipo katika hali nzuri hayupo duniani na hawezi kutokea
Kila mmoja anapitia matatizo katika maisha yake kwa nyakati tofauti
Ila huwezi kukaa bila tatizo hata moja
Matatizo ni kama mawimbi ya bahari ambapo kila siku yapo makubwa au madogo lakini lazima mawimbi yawepo tu
Utamaliza kutatua tatizo hili litakuja lingine na lingine na lingine kwa kifupi huwezi kuepuka matatizo bali unaweza kuepuka mtazamo hasi juu ya matatizo
Ondoa fikra kuwa matatizo yatafika mwisho haiwezekani
Huwezi kupanga nini kikutokee katika maisha yako bali unapanga ufanye nini kwa kile kimetokea
Kinachokutesa sio tatizo bali fikra zako juu ya kilichotokea
Tazama tofauti na utaona tofauti
2+2=4 ukitaka upate 5 fanya kitu tofauti
Kurudia jambo moja kila wakati na kutarajia matokeo tofauti hicho ni kichaa alisema Albert Einstein
Watu wengi hawana furaha kwa sababu wanaamini kila wanachopokea
Hawafikirii uhalisia wa vitu bali huwa wanahukumu hata kile hawajui lolote ndani yake
Ili uwe na furaha unatakiwa uende njia ya pekeako sio njia ya watu wengi
Watu wengi hawana furaha hivyo ukifuata njia zao unakuwa kama wao
Ongozana na watu 9 wenye hasira,wivu,chuki,kisasi, wasiosamehe,wenye kulalamika kisha utakuwa wa 10 wao
Watu wenye furaha hupata matatizo kama wasiokuwa na furaha isipokuwa hutazama uzuri tu katika kila tatizo linalokuja
Ukiona tatizo lipo nje ya uwezo wako liache
Ukiona tatizo lipo ndani ya uwezo litatue maisha yaendelee
Hofu haiwezi kuifanya kesho iwe tofauti na kujuta hakuwezi kuifanya jana irejee ufute kilichotokea
Kujuta sana haiwezi kubadilisha chochote na utazidi kuwa na hasira
Hasira ambazo haziwezi kubadilisha hali unayopitia hazina maana
Jipende sana kisha furaha yako jipe wewe
Mtu yeyote unatarajia akupe furaha atakuvunja moyo
Watu wanakuvunja moyo kwa sababu umeweka matarajio makubwa kwao kuliko uhalisia
Ondoa matarajio kwa watu kisha kubali chochote watafanya kisha pale unaweza kubadilisha badilisha kama huwezi acha
Huwezi kubadilisha akili za wengine, imani za wengine,tabia za wengine, matendo ya wengine ,hisia za wengine,maoni ya wengine
Hivyo kumbuka kitu pekee ambacho unamiliki kwa 100% ni akili yako tu
Kwa chochote utafanya kuna mtu atakuwa na mtazamo hasi juu yako
Huwezi kumpenda kila mtu na huwezi kupendwa na kila mtu
Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam