Unaishi ili ufanye nini?

Sasa kama wewe umeshindwa kukigundua unadhani kuna mtu atagundua kile unachotaka wewe?
Ndiyo huwa nafurahi lakini kuna kitu huwa nahisi hakijakamilika kila ninapotimiza jambo fulani. Nadhani hichi ndicho naweza kukigundua au kukielewa kutokana na maoni yenu.
 
Sijamaanisha kuwa nataka mtu mwingine agundue ninachokitaka ila ningependa tu kupata maoni tofautitofauti ambayo yanaweza toa mwanga kwangu mimi na wengine pia kuhusiana na malengo fulani.
Wewe unataka kugundua nini.
 
F

Fafanua tafadhari!
Kama ulizaliwa maisha yako ni nchi kavu lazma uishi ki nchi kavu nchi kavu huwezi ishi majini na ktk maisha uliyoyakuta au waliokutangulia huwezi tofautiana nao maana ulipozaliwa ulilelewa hadi ukijikuta ndo maisha yako hayo hivyo hukuwa na maamuzi yako kipindi uko mtoto na ndio maana upo kama ulivyo sasa hivi..
Ni sawa kwa sasa hivi nikuambiehamia sayari nyingine ambayo hujui utaanjia wapi maana hukujiandaa
 
Unaishi ili utimize kazi iliyokusudiwa na Mungu . Mf. Umsaidie katika kazi ya uumbaji , uache photocopy utakapotimiza maisha yako hapa duniani . Usivute oxygen bure ila uifanyie dunia kitu cha ukumbusho . Basi ishi ili utimize hayo
 
Kuna kitu kinaitwa MSUKUMO WA ASILI.

Huu msukumo wa asili au NATURE ndio unafanya mtoto akizaliwa anakimbilia kunyonya bila kufundishwa na yeyote, au hisia za kufanya mapenzi ambazo pia hafundishwi na mtu.

Hiyo hali unayoihisi ya kutokutosheka ndiyo inayomtofautisha binadamu na wanyama wengine na inampata kila binadamu, ambayo matokeo yake ndio haya maendeleo tunayoyaona duniani.
Binadamu tusingekuwa na hiyo hali, tungekuwa sawa na wanyama wengine na dunia isingekuwa na haya mabadiliko unayoyaona. Kwa kifupi tungekuwa tunaishi porini kama nyani.
 
Back
Top Bottom