Unaijua 2013 Subaru Forester SJ5?

Unaijua 2013 Subaru Forester SJ5?

Joined
Jan 20, 2026
Posts
78
Reaction score
108
2013 Subaru Forester SJ5 Ni gari ambayo imenunuliwa sana na inaendelea kununuliwa sana , ni gari yenye muonekano mzuri na wa kijanja haswaa!.

Iwe ni kwa kuendea shambani au mizunguko ya mjini, inatamba tu! ni gari yenye sifa kede - kede kutoka kwa watu wengi, kama vile kumpa mtumiaji ground clearance nzuri, nafasi pana ya kuwekea mizigo, na utulivu wa hali ya juu iwapo kwenye barabara hata za vumbi.

Huku ikiwa na vipengele muhimu vinavoipa mvuto zaidi kama vile camera nzuri ya reversing , CVT transmission, na X-Mode. Vitu vinavyoifanya kukuipa rating nzuri za kiusalama uwapo barabarani

Naam hiyo ndiyo 2013 SUBARU FORESTER! bwana!! Bei yake ikiwa utaagiza na @morning_joy_motors huwa ni TZS 31.5M Bei ikiwa imejumuisha pamoja na usajili!


Vipengele muhimu vya 2013 Subaru Forester (SJ5)


1. Utendaji wake wa kazi na Matunzo :

Hizi SJ series kikawaida zina body gumu zaidi na '' lower center of gravity'' yaani zina mwili na sura ya kigumu ( ya kazi ) ukilinganisha na matoleo yaliyopita, kuboresha utunzaji. Inajulikana kwa ubora wake wa uwezo kwenye mfumo wa , all-wheel-drive.


2. Ufanisi wa Engine & Utumiaji Mafuta :

2.0L petrol engine inakupa huukupa matumizi mazuri ya mafuta zaidi ukilinganisha na model zilizopita, huku baadhi ya watumiaji wakidai kutumia mafuta ya TZS 24,000/= kutembea hadi kwa kilometa mia moja, huku zinazotumia diesel zikiwa na ufanisi zaidi kwenye utumiaji wa mafuta kwa kutumia kiwango kidogo zaidi cha mafuta ukilinganisha na hii petrol!

3. Interior & Practicality :

interior yake ni pana zaidi , ikiwa imeboreshwa legroom na headroom, pia ikiongezwa, boot kubwa pamoja na siti za kuweza kukunjwa, na kwa model zingine zinakua na boot ya kufunguka na kujifunga yenyewe.

4.Usalama :

Hii gari inapokuja suala la usalama ilipata 5-star kwenye ANCAP rating, ikiwa na airbags saba, stability control, na, kwenye higher spec models, pamoja na driver assist system yaani EyeSight hivi vyote vikaifanya kujizolea nyote tano! Hata wewe mdau siumeipenda eeh!?


Naam, sasa mara baada ya kuona kuhusiana na uzuri wake tujikumbusha neno lile la wahenga kwamba hakuna kizuri siicho na kasoro. Sasa hebu tutazame kasoro zake pia na vitu ambavyo unapaswa uwe tayari kukumbana navyo.


Changamoto za kawaida ambazo ndio udhaifu mkubwa wa 2013 Subaru Forester SJG na namna ya kuzitatua


1. Inakula sana oil kupiata kawaida : Unapaswa kuwa nayo makini kwasababu mara nyingi huwa inatabia yakuchoma sana oil haswa hii yenye 2.5L.

Solution : Hakikisha unakagua mara kwa mara kiwango chako cha engine oil kuepuka kuharibu engine, na iwapo utakuta imepungua jitahidi kuongeza.

2. Matatizo ya CVT Transmission : Tatizo jingine kubwa la hii gari ni kwenye upande wa CVT transmission na dalili zake huwa pamoja na kutetemeka, kusitasita, au kuruka gears. Hizi ni dalili zake ambazo unapaswa kuwa nazo makini sana na kabla ya gearbox yako kufa, hivyo ni muhimu kuwa makini na kuiwahi.

Solution : Hakikisha mara kwa mara unaipima kwenye OBD machines na kuangalia software updates, weka transmission fluid original na hakikisha kila service unaifanya kwa wakati.

Kelele za sunspession za nyuma ama kufeli : Unaweza kuhisi kelele kama za kutetemeka kutokea kwenye sunspentio zako za nyuma, tatizo ambalo linaweza kuashiria kwamba bush zilizochakaa au , au wakati mwingine ikimaanisha spring za nyuma zilizokatika..

Solution : Hakikisha unakagua na kubadilisha bush za gari yako au struts.

Kuvuja kwa Engine Oil : Hii mara nyingi, kuanzia kwenye head gaskets, japo hii sio common kama ilivyo kwa model hizi za miaka hii ya karibuni.

Solution : Mara kwa mara hakikisha unakagua engine bay kuona kama kuna leaks napia hakikisha una - monitor cooling system.

Kunyonya Betri : Imekua pia ikilalamikiwa na baadhi ya watumiaji kwamba inanyonya sana betri.

Solution : Kagua alternator na hakikisha vifaa vyote vya umeme vimezimwa vizuri, mfano taa redio n.k pindi gari inapokua haitumiki.


Naam, sasa kazi ni kwako ndugu mdau kufanya uamuzi maana , sisi tumeshakufungulia ufahamu wa kumiliki unachokijua - Usishikishwe!!!!!


============================================================================


Karibu Morning Joy Motors.


KUHUSU MORNING JOY MOTORS

Morning Joy Motors
tunajihusha zaidi na ushauri, uelimishaji pamoja na uagizaji wa magari kwa muda wa zaidi ya miaka mitano hadi sasa.
Tunabeba dhamana kubwa ya ubora wa gari ambayo unaweza kuagiza kwetu kutokana na uzoefu wetu pamoja na ushirika wetu mzuri na wataalamu magari huko nje ambao kabla ya kuilipia gari ni lazima waifuate na kwenda kuikagua kwenye kila eneo kisha ndio kutupatia report ya kuendelea na utaratibu wa kuiagiza au la.

GUARANTEE : TUNAKUHAKIKISHIA UBORA, na USALAMA wa hali ya juu sana!
Na ikiwa sisi ndio tutakuchagulia gari na kisha ikakuletea shida, kwakua TUMEBEBA DHAMANA ya UBORA wa GARI yako na FEDHA YAKO
UTAIRUDISHA KWETU , NA UTAREJESHEWA FEDHA YAKO 100% PAMOJA NA FIDIA!

Hii ni kwasababu TUNAAMINI UBORA na UHAKIKA wa TUNACHOKIAGIZA na ndio maana TUNAJIAMINI na KUKUPA AHADI HII na HAITOKUA KWA MANENO TU BALI KWA VITENDO na MAANDISHI YA KISHERIA KABISA


KARIBUNI SANA


============================================================================


TUPO MKOA WA ARUSHA
KALOLENI KWENYE JENGO LA ARUSHA CONDO HOTEL
LILILOPO MKABALA NA SHALOM CHURCH
OFFICE NUMBER 016
GROUND FLOOR
SIMU : 0797113153 / WHATSAPP & NORMAL


============================================================================

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP
KWA ELIMU MBALIMBALI KUHUSIANA NA MAGARI PAMOJA NA UAGIZAJI
ANDIKA NENO '' MAGARI '' KWENYE WHATSAPP NUMBER 0797113153

Follow us on Instagram : @morning_joy_motors
follow us on facebook ; Morning Joy. Limited




Good Morning, The Joy Has Came!!!!!!
 
Back
Top Bottom