Unaiba nondo mradi wa maji?

unprejudiced

JF-Expert Member
Jan 27, 2017
3,505
2,862
Es gibt nichts Gutes, außer man tut es. Wanasema wajerumani.

Nimesikia huko kwetu mahali wananchi wameiba vifaa vya mradi wa maji. Sitegemei kuona uzi mrefu toka kwa wazalendo uchwara wanaodai demokrasia kuelezea ubaya wa mambo kama haya.

Kuna wakati najiuliza hivi maendeleo mnayoyataka bila wananchi wenyewe kuhusika yatatokea wapi? Nyie wambea na wadai fake wa demokrasia huwa hamyaoni haya ya msingi na kuyaandikia mauzi marefu au nyie ndo wahusika ili mpate cha kuandika.

Miradi ya maji ni changamoto sana kwa nchi maskini kwa kuwa ina gharama kubwa sana. Lakini inapofika kwetu ndo tunaanza kuichakachua.

Nawaambia ndugu, kwa tunayofanya kwenye public properties mbalimbali bila sisi binafsi kubadilika na kuwa responsible kwa matendo yetu hakuna kitakachofanikiwa na kudumu. Acheni kuandika mautopia. Changamoto za watanzania ni nyingi lakini kubwa ni kukosa respect kwa public properties.
 
unprejudiced

Kwa hiyo wewe unafikiri kinachofanya waibe nini? Ni matokeo ya sera mbovu za kuhakikisha watu wana kipato cha kutosha kupata mahitaji. So kabla ya kuwaandikia waswahili kijerumani waandikie wajerumani kiswahili uwaambie kwamba masisiemu hayana respect kwa public welfare and democracy
 
Kwa hio wewe unafikiri kinachofanya waibe nini?Nimatokeo ya sera mbovu za kuhakikisha watu wana kipato cha kutosha kupata mahitaji.So kabla ya kuwaandikia waswahili kijerumani waandikie wajerumani kiswahili uwaambie kwamba Masisiemu hayana Respekt kwa Public Welfare and Democracy
Mwizi ni mwizi tu

Hivi Mbowe anavyoiibia CHADEMA ni matokeo ya sera mbovu za CCM?
 
Hao wezi wameiba wapi na lini??? Mambo kama hayo ni kurudishana nyuma. Hao watu watafutwe wakamatwe washikishwe adabu.

Ova
 
Kwa hio wewe unafikiri kinachofanya waibe nini?Nimatokeo ya sera mbovu za kuhakikisha watu wana kipato cha kutosha kupata mahitaji.So kabla ya kuwaandikia waswahili kijerumani waandikie wajerumani kiswahili uwaambie kwamba Masisiemu hayana Respekt kwa Public Welfare and Democracy
Hivyo wewe Kiwete wa akili, unajua kipato cha kutosha watu kupata mahitaji yao kinatokana na nini? Kama hujui basi nakuomba kuanzia leo utambue kuwa kipato cha kutosha kina tokana na jitihada za watu kama wewe kufanya kazi kwa bidii badala ya kulalamika tu kila wakati. Na ndiyo maana Rais wetu anawahiniza watanzania kufanya kazi kwa bidii ili tuzalishe vyakula vya kututosheleza na ziada tuuze na kunua bidhaa ambazo sisi hatuzalishi.

Tanzania kama nchi yningi za Afrika na bara la Amerika ya kusini bado hatujafikia Standard ya maisha ya wamarekani na wazungu wa Ulaya ambao uchumi wao ni mkubwa kiasi kwamba kuwawezesha watu wao kuishi vizuri hata kama hawana kazi.

Uliishi kipindi cha Mwalim Nyerere baada ya vita na Uganda? Kamanulikuwa huja takiwa basi nakuomba mwuulize baba yako au mama yako au ikiwezekana babu au bibi yako nafikiri watakueleza hali ilivyo kuwa.

Sijawahi kuona katika maisha Tanzania kizazi ambacho kina uwezo mkubwa wa fursa za kujiendeleza binafi kama chenu. Lakini nasikitika maarifa hayo hamna. Mnataka kutafuniqa zu kila kitu.
 
unprejudiced

Kwa hiyo wewe unafikiri kinachofanya waibe nini? Ni matokeo ya sera mbovu za kuhakikisha watu wana kipato cha kutosha kupata mahitaji. So kabla ya kuwaandikia waswahili kijerumani waandikie wajerumani kiswahili uwaambie kwamba masisiemu hayana respect kwa public welfare and democracy
Nasikitika sana kuwamwona mtu kama Mayalla eti ana support huu uzi, kisa Rais Magufuli kamfukuza kazi au kam-demote mkuu wa TAKUKURU wa mkoa wa Mtwara kwa kuto kuwepo kwenye msafara wa Rais wilayani Masasi.

Jamaa nikimwangalia ninamsikitikia sana, yaani journalist aliyepata nafasi mbele ya watanzania na nchi nyingi za nje kwa kukaribishwa ikulu na kupewa fursa ya pekee ya kumwwuliza swali Rais, leo mwenyewe anajikunja ile mbaya na kudai eti Rais Magufuli hajamtendea haki huyo mkuu wa TAKUKURU wa mko.

Kwa ufahamu wangu inaonekana kuwa Mayalah yeye mateso ya wana Masasi wengi wanao kosa huduna za umuhimu kwa binadam maji na mengineo kqake yeye hata haijalishi, bali uamuzi wa Rais wa kumchukulia huyo kikaragosi papo kwa papo kwake ndiyo issue.

Hivyo yeye kama alivyo na kama binadam angekuwa katika Situation kama hiyo ya wana Masasi angejisikiaje? Yeye anacho jali ni haki ya huyo mtu mmoja wakati ambapo alitakiwa kwa mujibu wa sheria kuwepo katika huonmsafara. Hata kama ingeonekana kama ni mgonjwa au ghafla amepatwa na matatizo angemtuma mtu wa kumwakilisha. Au hata kutoa taarifa kwenye vyombo vinavyo husika.

Mayalah anatakiwa atambue kuwa huyo sokwe analipwa mshahara na umma kwa kutekeleza wajibu wake. Hafanyi hiyo kazi bure. Na hizo hela anazopewa yeye kwa kazi yake hiyo, kama mshahara, ni pesa ambayo sisi masikini tumejikunja katika kulipa kodi.

Inasikitisha sana kuona kuwa haki ya binadam mmoja, ambaye hatujui sababu zilizo mfanya yeye kuto appear kwenye msafara wa Rais, kuwa na uzito mkubwa sana kwa mtu kama Mayalla na wakoma wengine kuliko maisha na haki ya watoto, wazee vikongwe, vijana, viziwi na mababu, akina mama na akina baba ambao wanatakiwa kulijenga Taifa hilini, wanao ishi Masasi.

Is it justifiable?

Ina maana yeye Mayalla yuko tayari kuona maisha ya maelfu ya wana Masasi yana teketea maadam haki ya kiumbe kimoja inalindwa? Kwani hizo sheria na kanuni za haki za binadam zimeletwa na Mungu? Si sisi binadam wenyewe ndiyo tumejiwekea?

Sasa kama hizo kanununi za haki za binadam sisi wenyewe tumejitengenezea, haki ipi ina prevail nyingine, ile ya maelfu ya wana Masasi au ya kamanda mkuu mmoja wa TAKUKURU wa mkoa?

Mr Mayalla nafikiri utakumbuka hii picha iliyo pigwa na journalist mwenzako Kevin Carter wa Afrika ya kusini mwaka 1993 Kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan. Hii picha ili Trend sana ulimwenguni kiasi kwamba ilimsababishia Kevin kifo.
Kevin alijiua mwenyewe baadae baada ya kuona kuwa kitendo alicho kifanya sio cha ubinadam.

Kevin alitumia principles za u-journalism kuwa observor wakati ambapo angeweza okoa maisha ya huyo mtoto. Profession yake ilisababisha kifo chake.

Mayalla naye anafanya kile kile. Anatumia nguvu zake nyingi ku-defend right za binadam mmoja kwa kuyaona makosa ya Rais waka ambapo anasahau kuwa Rais naye anafanya hivyo hivyo kwa ajili ya maelfu ya wana Masasi.

Namwomna ndugu yangu Mayalla kuliangalia sana hilo. U-journalism wa sampuli hii unaweza ukampeleka pabaya. Akadhani anajenga kumbe anabomoa.

Hiyo inaonekana dhahiri kuwa huyo Bwana mkubwa wa TAKUKURU aliamua tu kuyeya, kwani alijua dhahiri kuwa kitu gani kinaendelea katika wilaya yao na Rais katika huo msafara atamnasa tu hana ujanja. Ndiyo maana akaamua kuingia mitini. Japo kuwa kama ilivyo kawaida yenu wanang'ang'ania vitu au tuseme kwa maneno mengine wanajaribu kulazima ukweli ambao haupo. Hatimaye wanaumbuka.

SmartSelect_20191017-113525_Gallery.jpeg
 
Back
Top Bottom