wadau napenda kuliona hili jukwaa la watu wanaopeana mbinu za kutatua matatizo na sio walalamishi, hivyo basi kama unawazo jipya la biashara liweke hapa au modify waliyoweka wengine.
Naanza mimi: ningekuwa na mtaji au kwa watu wenye mtaji naona kujenga vyoo kwenye barabara kuu sehemu ambazo watu huwa wanachimba dawa unaweza kuwa mradi mzuri, ni kwamba kila abiria kwenye gari analipia kama tsh mia mbili hivi kwa magari ya abiria na watu binafsi. Nahisi ni biashara ya uhakika sababu watu hawapendi kujisaidia wazi kama wanyama pia ni aibu wageni kutoka nje kuondoka na picha eti watanzania wanajisaidia hovyo. mwana jamii irekebishe hii au to wazo lako jipya hasa lisilo hitaji mtaji mkubwa.
hilo bado ni wazo sijatake even a single step, halafu kuifanya social interprise ni wazo ambalo nililifikiria pia, maeneo yale watu huwa wanauza na snacks kwa hiyo mnakuwa mnawezeshana kwa kuboresha mazingira ya biashara, hivi NEMC hawawezi kuhusika hapo?
mkuu
wazo zuri, siku hizi kuna style nyingi za ku-manage biashara ambapo lazima uwe na controlling tools za uhakika,
ningekushauri ufanye built and outsource operations,
hili wazo la kufanya outsourcing nimelipenda linaweza pia kupunguza worries tha Haika
Mie napenda sana kuwa na biashara yangu.
Tatizo nahisi kuwa nakuwa na vibes za negativity wakati wote.
naona vikwazo kuliko opportinities.
Mfano tu kwa mradi huu hapa naona kama itakuwa capital kubwa sana kusafiri hadi sehemu utakayoweka ofisi mara kwa mara kuisimamia. Ukijua kuwa Tanzania hii, biashara bila kuisimamia mwenyewe, ni kumuanzishia huyo mfanyakazi.
Naombeni msaada nitoke huku gizani
mkuu
wazo zuri, siku hizi kuna style nyingi za ku-manage biashara ambapo lazima uwe na controlling tools za uhakika,
ningekushauri ufanye built and outsource operations, jenga vyoo, weka standards zako za usafi na ada ya matumizi, tafuta mtu au kikundi cha watu mbalimbali, wape waendeshe hivyo vyoo kwa kuwapangia hesabu ya siku baada ya kuwa umeshaestablish kiasi cha mapato kwa siku kwa kufanya pilot study ya collections, hata wafanya usafi outsource, pesa yako iingie kwenye m-pesa kila siku, kama utakuwa na vituo katika njia za kaskazini, kati na kusini unaweza ukafanikiwa vizuri
assume njia ya kaskazini ina mabasi zaidi ya 40 yanayofanya safari kila siku
assume watakao tumia huduma hiyo ni 70% ya basi lenye abiria 60 - 42 passengers per day
42 x TZS 300 per person = 12,600
12,600 x 40 buses = 504,000
ukiwa na vituo 5 vyenye choo njia zote kubwa - 504,000 x 5 = 2,520,000 per day
weka mabasi madogo na magari madogo mengine katika vituo hivyo vyote yaingize 300,000 per day
total = TZS 2,820,000
chukua 40% ya kipato chote = TZS 1,128,000 per day
oooppppps, too good to be true
hebu na wadau wengine watoe mawazo yao
have a good day
Umeniibia wazo langu wewe,nimewaza hchi kitu miaka lakini huwa nasema watajenga 2 siku moja especially kutoka moshi kwenda dar,
Haa haa haa, unapaswa kujisifia kwa kutambua OPPORTUNITY (kwan kwa wengine ni kazi sana). Halafu kufanana mawazo si tatizo, tatizo liko hapo kwenye namna ya kuyaweka haya mawazo kwenye vitendo (UNIQUENESS). By the way mbona wewe hukulitekeleza hili kwa kipindi chote hicho? Au changamoto ndio ile ile anayosema RG? (Capital)
Hivi Mamzalendo kwenye hii Barabara (Dar- Arusha), ni sehemu gani watu wanapochimba Dawa kienyeji? Mbona Pale Msata (kwenye mizani) nimeona hii huduma? Halafu barabara hii inahoteli nyingi sana njiani, hivyo ni rahisi kupata hizi huduma (mfano Highway Hotel)
Umeniibia wazo langu wewe,nimewaza hchi kitu miaka lakini huwa nasema watajenga 2 siku moja especially kutoka moshi kwenda dar,