mimi nina msichana wangu ambae tupo kwa mda mrefu sana,katika miaka mingi tulio ishi tumejikuta tunapendana zaidi na kujiona tunaweza kuishi pamoja kama mke na mume,hivyo
tunajipanga ili tuwe pamoja kama mke na mume hapo baadae,kiukweli mimi nipo nae mbali kwa sasa yeye yupo dar nami nipo zenji kimasomo(chuo)na natarajia mwaka huu kumaliza masomo,na mungu akijaalia panapo uhai na uzima tutaenda kumchagua rais mpya tukiwa tumefuatana kama mke na mume.
kitu ambacho kinachoniumiza kichwa ni kwamba binti alipata wazo la kuenda VETA kupata ujuzi wa fani fulani,ila mie hakunishirikisha,akaenda kafanya mambo yake kamaliza alipopata na fasi ndio aliponiambia kwamba anataka kuenda VETA nikamuambia ni swala zuri sana,ila unataka kuchukua fani gani?akanijib nataka kuenda kuchukua fani ya hoteli,daaaa,mzee kichwa kiliniuma kusikia hotel,kwanza nilikua mbishi kidogo kumkubalia,maana mi najua mambo ya mahotelin,lakini kwakua binti ashapata nafasi akaniambia amelipiwa tuu na yeye anapelekwa tuu akasome,kishingo upande nikamuambia poa,kwakua tunaaminiana,
akanza chuo na alikua anaendelea vizuri,mpaka mwisho ulivyofika kamaliza akaenda field na akarudi kumalizia mitihani ya mwisho,hatimaye akapata cheti.
katika kuhangaika hapa na pale kutafuta kazi huwezi amin hata hajaniambia wala kunishirikisha pia,nilikua najua kama leo anaenda kufanya usahiri wakati nampigia sim mda mrefu hajapokea then akinitafuta ndio ananiambia kwamba alikua anafsnya usahiri,kwa bahati nzuri sasa amepata pa kujishikiza,tatizo liliopo anafanya kazi tabata yeye anakaa kigogo,anaingia saa 9 jioni anatoka saa 6 usiku au saba usiku,so mawasiliano kwa sasa yamepungua sana kwa kisingizio yupo kazini sim wanazima anatoka saa saba mie nishajipuunzisha,na asubuhi au mchana mimi nipo na mambo yangu ya chuo,siwezi kumcheki yeye,na kikubwa zaid mi hii kazi siikubali sana kwa mtoto wakike,then haswa kwa hizi shift za usiku,sasa hapo sijajua nifanye nini,
naombeni mawazo yenu wakuuuu