Tusiwalaumu, shule inachangia kwa kiwango kikubwa sana kwa hawa jamaa. Aliyetangaza kupanda kwa viwango vipya vya nauli ni Daktari wa kusomea, siyo wa kupewa, ni mtu makini na ambaye hana rekodi ya kushindwa katika wizara yoyote ile ingawa kimajungu inaonyesha huwa anapewa wizara usika ili ashindwe. Si lazima kila mtu akubaliane na mimi, lakini suala hili linabidi liangaliwe katika vigezo vifuatavyo.
1. Kwa kumbukumbu zangu, nauli ya Tsh 100 ilikuwepo tangu mwaka 1999 na sijui ilianza lini?
2. Kima cha chini cha mshahara kipindi hicho ilikuwa ni chini ya Tshs 17,000.00
3. Mkate kipindi hicho ulikuwa chini ya Tshs 250.00
4. Nauli ya basi kipindi hicho kutoka Mwenge hadi posta ilikuwa chini ya Tshs 150.00
5. Nauli ya basi kutoka Dar hadi Morogoro ilikuwa Tshs 3,000.00
6. Kilo moja ya sukari ilikuwa chini ya Tsh 600.00
7. Lita moja ya petroli ilikuwa chini ya Tshs 600.00
Vingi vingine mnaweza kuongezea, swali la msingi ni kuwa Je hawa wabunge wanafahamu gharama halisi ya vitu vyote hapo juu kimoja kimoja? vimepanda kwa asilimia ngapi kutoka kipindi hicho hadi sasa?
Ushauri: Wangekaa na Daktari, na wamuulize serikali inachukua initiative zipi kuboresha huduma za kivuko, na baada ya kuridhishwa ama kutokuridhishwa, wangewasilisha mapendekezo yao kwake huku wakiwaahidi wananchi wanafuatilia suala hili, na siyo kukinzana bila msingi na ni matumizi mabaya ta ofisi kwa kuwa hawatusaidii sisi wananchi ila ni malumbano ya mafahali na sisi nyasi tunaendelea kutaabika.
Nionavyo: Ulikuwa ni wakati muafaka, kuzungumzia high politics juu ya uuzwaji wa kigamboni na ujenzi wa daraja la kigamboni ambalo tangu lianze kuongelewa hadi leo halijaanza utekelezwaji wake.
Tuache majungu na kutafuta cheap popularity.