Exaud Mamuya
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 403
- 242
Hakika inaniwia vigumu sana kuwaelewa wabunge wa mkoa wa Dar kutokana na walichokiita kauli ya pamoja kuhusiana na uamuzi wa waziri wa ujenzi. Ndugu zangu hawa wamevalia njuga swala hili na kusema linawaumiza wananchi pasipo kujua wao walikuwa mstari wa mbele kutekeleza mambo makubwa sana yaliyowakandamiza wananchi hao hao ambao Leo hii wanajifanya wanawatetea. Mambo hayo ni Kama ifuatavyo: 1.Hawakujitokeza hadharani kwa umoja wao kupinga swala la DOWANS. 2.Walishiriki kikamilifu kupitisha muswada wa Katina mpya ambao ni ukandamizaji kwa wananchi. Leo hii mnawatetea wananchi gani kwa umoja wenu! Acheni unafiki.