Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Siku nzote nilikuwa mfwatiliaji mzuri sana wa huyu Mzee Ulimwengu kwenye vyombo vya habari tangu enzi za ,,Jenerali on Monday" mpaka kwenye makala za Gazeti lake la Rai enzi hizo, na siku zote makala zake zote alikuwa anaongelea tofauti ya Afrika na nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, kwa nini nchi kama Korea Kusini, Taiwani, Singapore zimeweza kupiga hatua kubwa ktk nchi za kipato cha chini kwenda kipato cha juu na alikuwa anasema ili Afrika tuweze kufika huko ni nini tunapaswa kufanya!
Jenerali Ulimwengu alikuwa anasifu aina ya utawala uliokuwa kwenye hizo nchi kama Korea Kusini tena alikuwa anatumia neno benevolent dictator ambalo kwa mara ya kwanza nililisikia kwake hivyo nilijifunza kitu ktk kwake, na hakuna kiongozi aliyekuwa anamsifu kama Raisi wa Korea Park Chung -hee na huyu alikuwa ni military dictator, yaani alipindua nchi kwa nguvu za Kijeshi ambaye yeye Ulimwengu alimuita benevolent dictator na alikuwa akienda mbali zaidi kusema kwamba ili Afrika iendelee tunahitaji Raisi kama Park wa Korea au Lee Kuan Yew wa Singapore, Kuonmitang (KMT) ambacho ni Chama cha kisoshalisti cha Taiwani kama vile CCM yetu!
Sasa ni ajabu J.Ulimwengu huyu huyu leo hii anasimama kwenye majukwaa na kutaka kuwa na Katiba mpya, Katiba ambayo itaiondoa madaraka makubwa ya Raisi ambayo ni muhimu ili nchi iweze kuendelea na hii ni kutokana na theory yake yeye mwenyewe Ulimwengu kwamba bila ya kufwata mfano wa Korea, Taiwani, Singapore hatuwezi kutoka, itahoji matokeo ya Uchaguzi Mahakamani ambapo kwa nchi changa na masikini kama yetu ni kosa kubwa sana kwa maana mkisharuhusu kuhoji matokeo Mahakamani hakuna kitakachofanyika kwani mwaka Miaka mitano yote mtaitumia Mahakamani mfano upo Kenya!
Hivyo hapa kuna mawili aidha Ulimwengu anatumiwa yaani ni mchumia tumbo au ni mtu asiye na msimamo na huwa anajiongelea tu ili kupata kiki ambayo ameipata kwa maana aliyoyasema mpaka Raisi amemjibu ingawaje siyo moja kwa moja ...