Ndugu zangu,
Hivi juzi kumetokea tukio baya la kuhuzunisha baada ya majangili wa tembo kumuua rubani wa kiingereza katika pori la akiba huko Simiyu mpakani mwa hifadhi ya Serengeti.
Ni wazi tukio hilo ni baya kwani limepoteza maisha ya binadamu mwenzetu lakini pia majangili hao walikuwa wamekwisha ua tembo mmoja katika eneo la tukio. Tunamuombea marehemu pumziko jema na ahueni kwa familia yake.
Ukiachana na tukio hilo, kilicho nikera ni unafiki wa baadhi ya watanzania kwenye mitandao ya kijamii (Twitter na FB) kujidai wanaumizwa sana na tukio hilo moja na kujisaulisha kuwa watanzania wenzetu askari wa wanyamapori wanauwa kila siku na majangili kwenye mapori na hifadhi za Taifa.
Sijawahi kuwasikia wakipost habari hizo za uzuni na kuguswa kwa wingi kama walivyofanya kwa kapteni wa chopa. Au kwa kuwa ndugu zetu hawa wanauwawa wakiwa kwenye malandlover na sio chopa? huu ni unafiki mkubwa.
Pili hao wanafiki wa mitandaoni wanatulazamisha kuamini kuwa kusimamishwa kwa operesheni tokomeza na bunge ndio kumesababisha majangili kuongezeka na sasa wanailamu bunge. Huu ni unafki mwingine mkubwa, nani asiyejua jinsi operesheni hiyo ilivyofanyika kwa unyama kwa mama zetu na picha za ushahidi zikiwawazi.
Nashauri tuepuke double standard kwenye masuala ya msingi, kiherehere cha kudai umeguswa na kifo cha kapteni mzungu kuliko askari wetu wa wanyama pori wanaokufa Selous, Katavi na Serengeti kila siku katika mazingira magumu kikome.
Inajulikana wazi mitandao ya majangili inahusisha watu wakubwa wenye nyadhifa kwenye chama na serikali, nguvu ielekezwe huko na tuthamini sana mchango wa watazanzania askari wazawa wanaovuja jasho kulinda rasilimali zetu.