Unafiki huu wa kujitoa ICC

Eti sisi bado tunashabikia, mbona hayo mataifa makubwa hayajiungi?
 
Ina maana hapa Tanzania mtu mwenye busara ndio Lowassa pekee....???

Tangu lini mwenye busara akawahadaa Watanzania Kuwa akichaguliwa kuwa Rais basi ndani ya siku 100 umasikini utakuwa Umekwisha.

Ndio busara hiyo.....???
 
Wao ndio wafadhili
Wao ndio walipa mishahara
Wao ndio wenye ardhi
Wao ndio wenye majengo
Wao ndio wenye miundombinu na facilities zote
Kuamini kuwa wanaweza kututendea haki .......

Waafrika wanaondoka sasa, hayo majengo watafuga kuku.
 
Ndio wafadhili
Kama mawazo yetu yatajikita kutegemea wafadhili na akili zetu zikategemea kuendeshwa na wakoloni tumekwisha. Hivi unafikiri tutaenelea na akili kama hizi mpaka lini? Ifike sehemu tuseme mwisho wa fikra tegemezi!
 
Kama mawazo yetu yatajikita kutegemea wafadhili na akili zetu zikategemea kuendeshwa na wakoloni tumekwisha. Hivi unafikiri tutaenelea na akili kama hizi mpaka lini? Ifike sehemu tuseme mwisho wa fikra tegemezi!
Sio kwa Africa ya sasa labda miaka 100 ijayo
 
Sio kwa Africa ya sasa labda miaka 100 ijayo
Iwapo watu wakiwa na mawazo kama hayo basi tumekwisha, tutaendelea kukosa viongozi kama kina Ghaddafi. Watauawa viongozi wetu wazuri kwa visingizio visivyo na mantiki, na wauaji wakiwa mikono salama kwa kuwa hawajasaini hiyo sheria ya ICC.
 
Nakosa jibu la kukupa, ila pole tu ambulia
 
Nyerere aliwah kusema, miti midogo porin iliona maboski ya mashoka yamebebwa yakipelekwa porin, ikaanza kupiga kelele, jaman mashoka. Miti mikubwa ikauliza yanakwenda wap? Miti midogo ikajibu yanakwenda porin. Miti mikubwa ikauliza tena je yana wajomba? Miti midogo ikajibu hapana, hayana wajomba. Miti mikubwa ikasema basi tulieni hayana madhara yoyote. Basi miti midogo ikatulia. Baada ya muda kupita mashoka yakaanza kurud kutoka porin yakiwa yamebebwa began ss awamu hii sio ktk maboski kama yalivyokwenda, miti midogo kama kawaida ikaanza kelele jaman mashoka. Miti mikubwa yako wap? Yana wajomba? Miti midogo ikajib ndio yanao wajomba tena yamebebwa began awamu hii, miti mikubwa ikasema ss tumekwisha.
Nn maana ya huu msemo wa Mwl Nyerere nafaham wazi kabisa kuwa wazee hawakumwelewa kabisa mzee huyu, alimaanisha kuwa wazungu hawawezi kuwadhoofisha waafrika bila kuwatumia waafrika wenyewe baadhi yao
 
We ndo mnafki namba moja,mbn Marekani anafanya maasi n hayupo ktk hiyo mahakama
 
We ndo mnafki namba moja,mbn Marekani anafanya maasi n hayupo ktk hiyo mahakama
Ndugu nazungumzia wale waliojiunga kwa spidi na sasa wanataka kujitoa, sikugusia kabisa ambao hawajawahi kujiunga
Ni vema ukasoma kitu ukakielewa kabla ya kukimbilia kujibu huko ni kukurupuka
 
Umeongea vizuri sana mkuu,..unatumia kinywaji gani aisee?...
 
Mkuu unatumia kinywaji gani?
 

Wauza silaha wakubwa duniani ni Wamarekani, wakifuatiwa kwa mbali na Warusi halafu ndio Wafaransa, Waingereza na Wajerumani:

1 United States $154.882 billion 41%
2 Russia $63.823 billion 17%
3 France $31.247 billion 8%
4 United Kingdom $26.914 billion 7%
5 Germany $16.261 billion 3%

The Top 5 Countries that Sell the Most Arms
 
Kaka ukisoma kitabu cha A Long Way Gone, utaelewa madhara makubwa ya vita. Vita ni uovu wa hali ya juu!! Na pia ni soko kubwa la silaha, madawa ya kulevya, biashara za magendo na binadamu, nk. Natamani kama hiki kitabu kingetafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ili wananchi wote wakisome! Sidhani kama kuna mtu atalilia vita akikisoma hiki kitabu. Baada ya kukisoma ukimsikia mwanasiasa yeyote analeta chokochoko ya vita au machafuko unaweza kumkimbiza kuliko mwizi.

Tamaa, ubinafsi na unafiki wa wengi wa viongozi wa dunia na asilimia kubwa ya wafanyabiashara wakubwa duniani, ndio huzaa migogoro na vita, huku wanyonge wakiathiriwa.
 
Wana sababu zao za kutisha sana na hii kitu inanipa hofu kubwa kwakuwa huko tuendako huko..!
Kiongozi tuendako ni hatari zaid zimwi kujifungua kamba?raia watakoma hakuna pa kuwashitaki yaani wao wanataka waue na wasishitakiwe
 
Wanataka kujitoa ili wawe huru kuwauwa wapinzani wao,huu ni ushenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…