Unafanya nini kumfanya mpenzio yule umtakaye?

Unafanya nini kumfanya mpenzio yule umtakaye?

bigmind

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2015
Posts
12,457
Reaction score
12,714
Leo naomba niwashukie kama mvua wakaka na wadada hasa wale wenye wanaume/wanawake wa ndoto zao. Ingawa mara nyingi hali imekuwa tofauti na mategemeo yao na kubaki kulala mitandaoni na kulaani bila kujitazama wao wanawajibika kiasi gani.

Naomba niwaeleze kitu kimoja iko hivi mpenzi wako alivyo anareflect wewe ulivyo maana kama haufanyi jitihada za kumbadirisha kimtazamo, kimwonekano na kimawazo usitegemee from no where awe kama unavyopenda awe.

Niwaibie siri dada zangu, mliowengi mnajiona kuwa nyie ni viumbe duni na huwa mnatembelea akili za mabwana/boyfriend zenu sasa omba awe kichwa la sivyo utakuja siku moja na magunia ya malalamiko hapa. Mwanaume anapenda kuongoza lakini uwezo wetu juu ya maisha hatuko vizuri na tunapendezwa sana na wanawake wanaotoa ushauri juu ya maisha.

Nani asiyejua kuwa sisi wanaume ni wavujaji wa mali kwa kuonga, na anasa za kijinga, ila utamkuta mwanamke anajisifia kuwa na mwanaume anayeonga na kuwasifia wanaume waongaji ila siku akigundua mumewe kapenda sehemu nyingine anaendeleza ukarimu uleule wa kuonga na kutumia pesq bila mpangilio anatokwa na povu mpaka basi.

Hakika nakwambia ukijidai kutafuta mwanamke/me aliyekamilika ukasahau mnatakiwa kukamilishana ujue utasubiri mno na utazeekea kwenu.

Kila mmoja afanye kazi ya kumbadilisha mwenziwe mtafanikiwa vizuri sana, mambo ya kutupiana lawana bila kuchukua hatua utaachika ewe mdada mpaka uhisi una nuksi/mkosi kumbe ni mambo tu ya kujituma na mwenzio angekuelewa. Awe mkaka kabla haujachukua maamzi ya kumwacha mdada fanya juhudi za kumbadilisha kuwa yule umtakaye. Hakikisha unawajibika katika mahusiano, kaa panga wote kufanikiwa ni rahisi na ni njia rahisi ya kupunguza manyanyaso hasa ya kijinsia.

Nawapenda wana MMU wote mbarikiwe.
 
interesting....... ila limekosa wachangiaji coz si mahala pake,,,,, wengine hadi huku chumbani hawafikagi.
 
Kila siku nasema hivi
1475168695480.jpg
 
Back
Top Bottom