Unafahamu hili??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafahamu hili???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mcubic, Aug 19, 2012.

 1. mcubic

  mcubic JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 10,160
  Likes Received: 4,183
  Trophy Points: 280
  Eid Mubarak wana JF. Pamoja na kuwa leo ni mapumziko ya siku kuu ya Eid, si vibaya nikaletea taarifa hii ili muikosoe au hata kutoa mitazmo yenu. Wizara ya kilimo, chakula na ushirika ina idara nyingi, mojawapo ya idara hizo ni utafiti na mafunzo.

  Zamani idara hizi zilikuwa pamoja na baadaye kutenguliwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuongeza ufanisi na tija katika kilimo. Jambo linaloshangaza kwa sasa ni kupishana kwa mishahara kwa kiwango kikubwa kati ya watumishi wa idara ya utafiti na ile ya mafunzo, sababu inayotolewa kuwa watafiti wana kazi ngumu sana ukilinganisha na wafanyakazi wa kada nyingine katika wizara hii moja.

  Vijana wanaoajiriwa sasa hivi wamekuwa wakipigania kuajiriwa katika idara ya utafiti kuliko idara nyingine kufuata malisho mema yaliyo huko. Vijana hao ambao wengi wanamaliza SUA katika ngazi ya degree na hata kufanana kwa madaraja ya ufaulu, daraja la utenganisho huanza hapo, kwa watakaobahatika kupata utafiti mambo huwa poa, ukibahatika kuingia idara nyingine, unaingia kwenye kundi la walalamikaji.

  Mtafiti anatafuta teknolojia madhubuti na yenye tija katika kilimo na ni jambo muhimu katika maendeleo ya nchi yetu. Lakini mtafiti huyu mpaka afikie lengo lake yampasa kuwashirikisha watu wengi hapa katikati ili teknolojia imfikie mlengwa. Mathalani mkufunzi kilimo anakuwa na lundo la wakurufunzi, kuwapa utaalamu ama kuwaelekeza teknolojia mbalimbali zilizotafutwa na mtafiti, nia na madhumuni ni wakurufunzi hao kufikisha teknolojia hiyo sehemu husika.

  Shida yangu mimi ni hapa je ni halali kwa watu hawa kutofautiana viwango vya mishahara mara tatu ama nne? ukizingatia wote ni wataalamu, hali hii haivunji morali ya kufanya kazi, na kufanya vijana wasipende kuajiriwa katika idara nyingine? Nini Kifanyike kubadilisha hili.

  Maoni yenu ni muhimu....
   
Loading...