Unadhani Suleiman Leo angekuwa Rais wa Afrika angeomba hekima? Marais wenzie wangemcheka sana

Guru Master

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
224
591
Kama kuna moja ya watu wapuuzi kabisa kupata kutokea duniani alikuwa ni mfalme selemani/solomon. huyu alipata bahati ya kuambiwa na Mungu aombe kitu chochote atakacho toka kwa Mungu. hii ilikuwa bahati ya mtende kuota jangwan. lahaaaulah... huyu mfalme mpuuzi aliomba hekima. hekima? unaomba hekima? we mfalme seleman ungekuwa afrika halafu ukapata wasaa wa kunena na bwana Mungu ukaomba hekima na viongozi wenzio au marais wengine wangekusikia wangekucheka sana kwa kuonesha kiwango kikubwa sana cha Ujuha.

unaomba hekima? hekima itakusaidia nini kuongoza waafrika? ungeomba utajiri. ungeomba mali, ungeomba utawale milele au ungeomba wapinzani wako wafe tena kwa vifo vibaya kabisa. ndiyo ungewaombea mabaya tu kuwa akijitokeza mtu anataka kukupinga Mungu amuue haraka sana au wa mateso makubwa sana ili iwe fundisho kwa wengine.

afrika inataka viongozi wasio na hekima. viongoz wababe, wenye chuki, wenye kusambaza chuki, wanazi wa vyama vyao na ambao wapo tayari kufia vyama vyao. afrika kiongoz anaweza simama akahutubia akisambaza chuki na mgawanyo katika taifa na wanaomsikiliza wakashangilia wakisema "sema babaaaaaaa" haya yanatokea afrika tu. kwa wenzetu ni ngumu sana si kwa kiwango hiki kinachotokea kwetu.

sifa za kiongozi wa afrika..
1. uwe mbabe/ dikteta wewe ndo mwamuzi wa mwisho
2. uwe mzuri sana akwa kuongea maneno ya mipasho
3. uweze kujiundia kakikundi mabcho wote mtafisadi nchi
4. uwe na uwezo wa kujitengenezea mazingira mazuri ya kuwa karibu na polisi na wanajeshi ili hawa wakulinde dhidh ya wananchi
5. usiwe na huruma kwa wapinzani wako, wafunge,watese,wapoteze,waue,wadhalilishe
6. uwe na genge la watu wako ambao wao watakusikiliza unachosema na kukifanyia kazi ili kulinda maslah yenu.

ukiangalia sifa hizo huoni suala la hekima. hekima ya nini? unaomba hekima ili iweje? na ndo maana ukiangalia viongoz wetu wengi wakiwa wanahutubia utagundua hawana hekima. wawe kwenye mikutano ya kuomba kura, bungeni au mikutano ya ndani na nje ya kawaida kama wanasiasa.utagundua hawana hekima, hawana busara. na hawahitaji.

Mfalme solomoni alijua alipaswa kuwatawala watu wale kwa hekima na si ubabe,nguvu,ujivuni,utajiri,chuki na uovu.
"WAKISHINDWA KUOMBA HEKIMA TUWAOMBEE HEKIMA"
 
Inawezekana hujaelewa muktadha wa sala ya kwenye njozi ya Solomon. Utawala wake ulikuwa umechukuliwa na kaka yake mpaka baba yake Mfalme Daudi alipoweka mguu chini kuwa Solomon ndiye anatakiwa awe Mfalme baada ya Daudi. Kwa hiyo Solomon aliomba hekima kwa sababu ulikuwa ndiyo mtaji ambao ungemwezesha kutawala na kupendwa na Waisraeli.
Pili, Mwenyezi Mungu wakati wa kujibu sala ya Solomoni alimpa, kwa maelezo dhahiri, hata yale ambayo Solomon hakuyaomba: Alimpa maisha marefu na mali nyingi. Mwenyezi Mungu alisema kuwa alimpa hayo kwa sababu Solomon hakutumia nafasi ya sala yake kuwaombea adui zake mabaya.
Tofauti na Ma-Rais wengi au Viongozi wakuu wa Afrika, hudhani kuwa watu wao wengi wakiwapigia kura za kushika madaraka basi hii ni cheti kuwa wana hekima na busara kuliko ye yote mwingine kwa hiyo hawatoi nafasi ya wao kukusanya mawazo mazuri na uzoefu uliopo ili kuendeleza taifa husika. Kwa maana hiyo wanaturudisha nyuma kwa kuanza majaribio ya hekima na busara zao binafsi ambazo ni za kawaida tu au hata hafifu zaidi na hivyo kukosa fursa ya kuendeleza taifa husika.
Hilo la kumwomba Mungu kwa dhati kama Solomon ndiyo halipo kabisa. Kanisani au Msikitini ni kwa ajili ya kupata nafasi kwenye habari hasa za TV. Sana sana Mganga wa kienyeji, shanga, pete. mikufu na hirizi, kwa kifupi, ushirikina vinaweza kupata nafasi kubwa zaidi. Sio wote ila wengi wao.
Hayo ndiyo matatizo ya Waafrika wetu.
 
Back
Top Bottom