Unaamini majina yanaathiri watoto kama tunavyoyapa uzito?

msakhara

JF-Expert Member
May 26, 2019
271
370
Kumekua na dhana ya muda mrefu ya kwamba jina analopewa mtu huwa lina athiri haiba yake. Hii inapelekea watu kuwapa watoto wao majina yanayoambatana na watu waliofanikiwa ili wafanikiwe pia.

Lakini pamoja na hayo nimekua nikiona kunabaadhi ya watu hawaendani na majina. Mf. unakuta mtu anaitwa Isaya, ni mwizi, Mohammed ila tapeli au Ronald bangi sana ama Maria mcharukooo.

Wewe unaamini majina yanaathiri watoto kama tunavyoyapa uzito? Kwanini?
 
Kama huamini basi muite mtoto wako majina haya ; Huruma, Mateso, Masumbuko, Mtumwa, Kijakazi, Shida, Chuki, Chausiku, nk. halafu uone!!!!
 
Mimi naamini majina hayaathiri watoto kama tunavyoyapa uzito.


Na kama ukisema majina yanaathiri kama tunavyoyapa uzito, Hapo inaweza ikaibuka hoja nzuri kidogo.

Mfano kwenye vitabu vya dini, nyakati zetu kuna watu wana majina ya kwenye vitabu vya dini, ambapo matendo yao hayaendani na yale yaliyoandikwa kwenye vitabu.

Inawezekana tabia walizonazo akina James Delicious ndizo tabia halisi za akina James wa kwenye kitabu.
 
Kama huamini basi muite mtoto wako majina haya ; Huruma, Mateso, Masumbuko, Mtumwa, Kijakazi, Shida, Chuki, Chausiku, nk. halafu uone!!!!
Umenikumbusha kuna ndugu yangu anaitwa Hasara, alikuwa safarini na jamaa yake anaitwa Matatizo.

Sasa njiani wakakutana na askari wa barabarani Trafiki.
Walikuwa wanatumia usafiri wa pikipiki,

Walikutwa na makosa kadhaa madogo baada ya kukaguliwa.

Sasa trafiki alipomuuliza dereva anaitwa nani, akasema anaitwa Hasara,

alipo muuliza mwenzie anaitwa nani, akasema anaitwa Matatizo.
Trafiki akasema, kwahiyo wewe ni Hasara na huyu mwenzio ni Matatizo?

Trafiki akabaki anacheka na akawaruhusu waendelee na safari yao.
 
Umenikumbusha kuna ndugu yangu anaitwa Hasara, alikuwa safarini na jamaa yake anaitwa Matatizo.

Sasa njiani wakakutana na askari wa barabarani Trafiki.
Walikuwa wanatumia usafiri wa pikipiki...
 
Back
Top Bottom