Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,374
- 38,248
Wengi wetu tumekuwa huku tukiaminishwa kuwa hasira ni kitu kibaya sana, na si mara moja ama mbili, tumekuwa tukiwalaumu watu kwa kuwa na hasira. Hata washahili hawakubaki nyuma, nao wamekuwa na misemo, kama vile: HASIRA HASARA, HASIRA ZA MKIZI
.! Hii yote ni kulaani ama kuwazodoa watu wenye hasira. BInafsi simlaumu mwenye hasira!
Najua unajua, ila ninegependa kukujuza zaidi kuwa, hasira zina faida sana katika maisha yetu ya kila siku kuliko vile ambavyo wengi katika jamii, wanachukulia!
Hizi ni faida chache tu, nimependa kukuongezea katika zile unazozijua!
Hasira huleta maridhiano
Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana. Kuna wakati watu hawawezi kuheshimiana au hata kufikia makubaliano fulani, mpaka mmoja wapo apandishe hasira. Hasira huleta muafaka. Mfano: Wanandoa, wanaweza kuishi pamoja kwa muda mrefu, lakini ikafika mahali, mmoja akaona hana tena Maslahi na ndoa ile, anaamua kiroho safi tu, kuomba poo, anangatuka, anaomba kujiomndoa! Inatokea upande wa pili kupinga wazo hili, lakini huyu huyu mpinzani, ipo siku atakubaliana na wazo la mwenzake baada ya mwenzake kuonyesha hasira alionayo dhidi yake! Hapa muafaka hupatikana kwa mmoja kukubali basi yaishe, talaka yako hii hapa!
Hata haya madeni tunayodaiana maofisini na uswahilini, kuna wakati mnufaika hulipwa chake baada ya kuonyesha kiwango Fulani cha hasira!
Hasira ni kichocheo:
Kuna baadhi ya mambo huwa hayaendi mpaka mtu apate nguvu ya ziada itakayomsukuma kufanya kile kitu. Hasira inaweza kuwa kichocheo cha wewe kufanya kile ambacho bila ya nguvu ya ziada usingekifanya. Mfano: upo katika mahusiano na mtu ambae, kwa sasa umeshakiri kuwa huwezi kuendelea nae, tayari umeshafikiria kuachana nae1 changamoto ulionayo ni kwamba, umekosa nguvu ya ziada ya kufanya uamuzi. Katika hali hii unahitaji siku na saa tu, upatwe na hasira (kichocheo) dhidi ya mtu huyu, na hatimaye kufikia dhumuni lako. Hapa hasira imekuwa na faida kwako!
Hasira ni njia sahihi ya mawasiliano:
Kuna maswali unaweza ukajiuliza wewe mwenyewe! Katika watu wanaokuzunguka, wangapi wanakuogopa? Katika hao, ni wangapi wanakuogopa kwa sababu ya hasira zako? Katika hawa ambao wanakuogopa kwa hasira zako, ni lini na wakati gani uliwaambia kuwa wewe una hasira? Ni mangapi yamekupita ama hukufanyiwa na watu wanaokuogopa? Hapa jibu ni kwamba, hasira zako zilituma ujumbe kwa watu hawa kuwa wewe ni mtu wa aina Fulani, na si mtu wa aina ile, mf: wewe si mtu wa kutapeliwa, kubezwa, masihara, ujinga au kwa kifupi wewe sio lofa!
Hasira huleta kujitambua:
Ni wangapi tunataka mabadiliko mwaka huu? Ni wengi tu! katika wengi tunaotaka mabadiliko, kila mtu ana sababu yake ya mabadiliko. Lakini ukweli ulio wazi ni kuwa, katika hawa wanaotaka mabadiliko, kuna wenye hasira zao na ndio kisa cha kutaka mabadiliko, wana hasira na mfumo wa maisha uliopo sasa hivi! Wana hasira dhidi ya watu wale wale! Hasira zimewafanya watu hawa kujitambua!
Hasira hupunguza ukatili:
Nakuona ushajiandaa ni kupinga. Ni hivi. Hasira huleta ukatili ama hata unyama. Katika hali ya kawaida, hasira hujidhihirisha wazi wazi baina ya wahusika, watu wanaowazunguka wanapoona wahusika wana hasira, wanajua baada ya moshi moto, ana kifuatacho baada ya hasira ni vita, watu wanaowapenda huingilia kati ili kuepusha shari au madhara. Hawaluitwa kuja kuamulia fukuto, ila hasira za wahusika zimefanya watu wajiongeze na kuja kuwasuruhisha kabla ya madhara hayajawa makubwa, hivo ndio kusema kwa hapa, hasira imeepusha majanga zaidi!
Hizi ni zangu mimi, na wewe ongezea za kwako, kama mbayuwayu!