UN kupigia kura mswada kuhusu Jerusalem

UN kupigia kura mswada kuhusu Jerusalem

Chillah

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2016
Posts
9,506
Reaction score
10,872
UN kupigia kura mswada kuhusu Jerusalem
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatafakari kupitisha mswada unaosema mabadiliko yoyote ya hadhi ya mji wa Jerusalem hayatakuwa na athari kisheria na yanapaswa kubadilishwa.


Balozi wa Misri katika Umoja wa mataifa Abdellatif Aboulatta

Misri imesambaza mswada huo Jumamosi (16.12.2017), na wanadiplomasia wamesema baraza huenda likapiga kura kuhusiana na mapendekezo hayo mapema hata Jumatatu.

Akijitoa katika mwelekeo wa kimataifa , rais wa Marekani Donald Trump mwezi huu alitangaza kwamba atautambua mji wa Jerusalem katika mji mkuu wa Israel na kuhamishia ubalozi wa Marekani katika mji huo kutoka Tel Aviv, hatua hiyo imezusha maandamano na shutuma kali.


Maandamano ya kushutumu hatua ya Marekani kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Mswada huo wa azimio uliopatikana na shirika la habari la AFP unasisitiza kwamba Jerusalem ni suala , "ambalo linaamuliwa kupitia majadiliano" na kueleza "masikitiko makubwa katika uamuzi wa hivi karibuni kuhusiana na hadhi ya mji wa Jerusalem," bila kutaja moja kwa moja uamuzi wa rais Trump.

"Uamuzi wowote na hatua ambazo zitaonekana kubadilisha hadhi, hali na jamii iliyopo katika mji huo mtakatifu wa Jerusalem havitakuwa na athari ya kisheria, na ni batili na ni lazima ubadilishwe," mswada huo umesema.

Wanadiplomasia wanasema wanatarajia Marekani kutumia uwezo wake wa kura ya turufu kuzuwia hatua hiyo wakati , wengi kama sio wote , wajumbe 14 wa baraza la Usalama wanatarajia kuunga mkono mswada huo wa azimio.


Maandamano Gaza kupinga hatua ya Marekani kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Pence kwenda Mashariki ya kati

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence atazuru Jerusalem siku ya Jumatano , akijitumbukiza katika mzozo wa moja kati ya suala lenye utata kabisa katika mzozo kati ya Wapalestina na Israel.

Israel ilichukua udhibiti wa sehemu ya mashariki mwa mji huo katika vita vya mashariki ya kati mwaka 1967 na inaliona eneo lote la mji wa Jerusalem kuwa mji ambao haukugawanyika.


Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence

Wapalestina wanaliona eneo la mashariki mwa Jerusalem kuwa mji mkuu wao wa hapo baadaye.

Balozi wa Israel katika Umoja wa mataifa Danny Danon "anashutumu vikali" mswada huo , akipuuzia kwamba ni juhudi za Wapalestina "kuandika upya historia."

"Hakuna kura ama mjadala utakaobadilisha hali halisi kwamba Jerusalem ilikuwa ama itakuwa mji mkuu wa Israel," danon alisema katika taarifa.

Mswada huo wa azimio unatoa wito kwa nchi zote kujizuwia kufungua balozi zao mjini Jerusalem, ukiakisi wasi wasi kwamba serikali nyingine zinaweza kufuata kile Marekani ilichofanya.


Rais Donald Trump wakati akitoa tamko la kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Mswada huo unataka kwamba mataifa yote wanachama kutotambua hatua yoyote ambayo itakwenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu hadhi ya mji huo.

Maazimio kadhaa ya Umoja wa mataifa yanaitaka Israel kujiondoa kutoka katika ardhi iliyokamata wakati wa vita vya mwaka 1967 na kusisitiza haja ya kufikisha mwisho kulikalia eneo la Wapalestina.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Isaac Gamba

UN kupigia kura mswada kuhusu Jerusalem | Matukio ya Kisiasa | DW | 17.12.2017
 
Trump baada ya kuutambua Jerusalemu kama mji mkuu wa Israel kakaa zake kimya upande mwingine jamaa wakaanza gombana
 
Trump baada ya kuutambua Jerusalemu kama mji mkuu wa Israel kakaa zake kimya upande mwingine jamaa wakaanza gombana
Ha ha ha ha ha! Duh! Statement ya Trump kuutambua Jerusalem was among the shortest statements ever matokeo yake pande zote za dunia wanawashwa. Jamaa wala hana hata habari yuko mapumzikoni akijiandaa zake kula Xmas na New Year huko Camp David na kwingineko kwenye ranch zake akicheza zake hockey, michezo ya farasi, na kuteleza kwenye theluji.
 
hawa watoto wa kijakazi sijui tatizo lao nini.... mji uko nchi nyingine afu wengine wana washwa washwa kuhusu huo mji eti ni wa ndugu zao....
kama ni wa ndugu yenu nendeni mkamsaidie kuuchukua
 
hawa watoto wa kijakazi sijui tatizo lao nini.... mji uko nchi nyingine afu wengine wana washwa washwa kuhusu huo mji eti ni wa ndugu zao....
kama ni wa ndugu yenu nendeni mkamsaidie kuuchukua
We unasema hao tu wanawashwa whawa waisrael weusi huwaoni wanavyojikuna hovyo huku?
 
Back
Top Bottom