UN: Idadi ya watu wanaohitaji msaada duniani yaongezeka

UN: Idadi ya watu wanaohitaji msaada duniani yaongezeka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
Umoja wa Mataifa umesema mmoja kati ya watu 45 duniani ambao ni sawa na milioni 168, watahitaji msaada wa kibinadamu ifikapo mwaka 2020.

Kwa mujibu wa ripoti ya umoja huo idadi ya watu wanaohitaji msaada imeongezeka hadi milioni 22 katika kipindi cha mwaka uliopita kutokana na migogoro na machafuko ya muda mrefu, majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kusuasua kwa uchumi.

Katika mapitio ya kila mwaka kuhusu hali ya kibinadamu duniani, Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali umesema unakusudia kuwasaidia watu milioni 109 walioko hatarini zaidi katika nchi 55 mwaka ujao, hivyo unahitajika msaada wa kiasi cha Dola bilioni 29.

Taarifa hiyo imezitaja nchi zilizo na hali mbaya zaidi kuwa ni pamoja na Yemen, Syria, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Somalia, Sudan Kusini na Sudan.
 
Hawa jamaa kumbe na wenyewe wanahitaji msaada waweze kuwasaidia wanaohitaji msaada?

Wanakuaga na report nzuri sana, takwimu tamu, maandishi yenye bashasha lakini utekelezaji wa hizo report unasuasua sana.

Mfano waliwahi kuja na ngonjera za MDG.
Sasa hivi wanaimba SDGs..
Kuna matamko mengi tu yanaongelea hatari za uchafuzi wa mazingira kwenye tabia nchi.
Utawala bora na haki za binadam. Cha ajabu hali inazidi kuwa mbaya, inafika mahali unajiuliza hii mikutano, matamasha, na matamko yanatija kweli au kutimiza wajibu tu?
 
Back
Top Bottom