mbinguni
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 2,767
- 1,068
Ni dhahiri kabisa kuwa sasa ndio muda muafaka wa kuikataa na kuizika rasmi ccm.Matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa jana yanadhihirisha kuwa ccm na serikali yake ni dhaifu(John Mnyika).Migomo halali ya walimu na kada nyingine za wafanyakazi juu ya mustakabali wa mishahara yao iliyopingwa kwa nguvu ya mahakama kuwa sio halali imetuonyesha uhalisia wa serikali hii DHALIMU isiyojali kabisa ubora wa maisha ya wananchi wake.Ifike mahali sasa watanganyika tuwakatae hawa wakoloni weusi kwa njia yeyote ile.Mfano mzuri ni hoja ya msingi ya mbatia kukataliwa kiushabiki na bunge la hawa ccm.Wao maslahi ya umma nyuma na maslahi yao (ccm) mbele.Kila mmoja popote alipo tuunganishe nguvu zetu tuikomboe nchi yetu hapo 2015.