Umuhimu wa kusoma vitabu

Umuhimu wa kusoma vitabu

Tanzanian-1

Member
Joined
Feb 25, 2018
Posts
6
Reaction score
5
Habari za muda huu chiefs?

huu ukiwa ni uzi wangu wa kwanza kupost humu JF naomba niongelee suala la usomaji wa vitabu, japo tayari wapo waliokwisha liongelea naomba namm nilipigilie nchi sita.


kusoma vitabu kuna manufaa mengi kwa mtu binafsi na
kwa jamii pia.

Tunaweza kuitafakari kauli hii kwa
namna nyingi.
Binafsi, daima ninakumbuka usemi
wa Jamaa anaitwa Ernest Hemingway, yeye alisema "There is no friend more
loyal than a book," yaani hakuna rafiki wa kweli
kuzidi kitabu.
Ni kauli fupi na rahisi kukumbukwa,
lakini ninaiona kuwa yenye ukweli kabisa.
Kitabu ni rafiki ambaye yuko kwa ajili yako muda
wowote unapomhitaji. Kitabu kinaweza kuwa
mshauri wako, kiongozi wako, nguzo ya
kuitegemea.
Akili ya binadamu inahitaji matunzo, sawa na
bustani. Bustani inahitaji kurutubishwa na
kupaliliwa. Ikiachwa ivamiwe na magugu, inageuka
kichaka. Kusoma vitabu ni kurutubisha akili na
kuipalilia. Kama mtu anaweza, ni muhimu kusoma
vitabu vya aina mbali mbali: vya siasa, saikolojia,
fasihi, sayansi, maisha ya watu maarufu, falsafa,Mungu,
historia, uchumi, na kadhalika.

Ni makosa kudhani kuwa kusoma vitabu
kunawahusu wanafunzi na waalimu pekee. Kila mtu
anapaswa kusoma vitabu kwasababu vitabu vinatusaidia yafuatayo :-

*Kuelewa mambo mapya ambayo tulikua hatuyajui.

*mawasiliano baina ya vizazi

*Kuongeza ujuzi wa ziada maishani mwako

Na mengine mengi tu
Tutafakari manufaa
yake kwa afya ya akili ya binadamu.
 
Back
Top Bottom