Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,070
- 151,323
Katiba ya mzee Warioba ilikuwa na kipengele kilichokuwa kinawataka viongozi wa umma kutopokea zawadi na kukaa nazo kama mali zao binafsi na badala yake kipengele hicho kiliwataka viongozi wa umma kukabidhi zawadi hizo serikalini. Hii ni kwa mujibu wa kumbukumbu zangu na kama kumbukumbu zangu si sahihi niko tayari kurekebishwa.
Naomba nikiri mzee Warioba na Tume yake kwa kutumia maoni ya wananchi walifanya kazi yao kwa weledi wa hali ya juu sana na sidhani kama Katiba inayayopendekezwa inabeba kifungu hiki.
Sasa wadau leo hii Magufuli kama Rais anapewa zawadi, kesho anaweza akawa Makamu wa Rais na kesho kutwa akawa Waziri fulani.
Je, zawadi za aina hii kupewa viongozi hazina madhara?
Kwa mfano, kesho na keshokutwa waziri akizawadiwa vipande vya "dhahabu" au "almasi" na makampuni ya ndani ya uchimbaji wa madini, nani atahoji iwapo Raisi ataamua kukaa na n'gombe hao kama mali yake binafsi?
Waziri aliepokea zawadi kama hiyo ataweza vipi kutimiza majukumu yake kama waziri kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi iwapo kampuni iliyomzawadia itabainika kuvunja au kukiuka sheria za nchi katika shughuli zake za uchimbaji wa madini?
Zawadi za aina hii kwa viongozi ni jambo jema lakini wakati mwingine zinaweza kuwa na madhara kiutendaji kama vile kumfunga mdomo kiongozi n.k.
Tuirejee katiba ya mzee ya Warioba kwa manufaa ya nchi hii.