Umuhimu wa Digital Security

LONE_WOLF

Senior Member
Joined
Nov 21, 2015
Posts
175
Reaction score
260
Bazazi habari ya mda huu, bila kuchelewa niongelee suala hili muhimu kwa watu wangu makini sana. Tunatambua kuna ongezeko la social networks hasa playstore, appstore na kwenye web browser. Upatikanaji huu unakuja na risk zake hasa kudukuliwa account e.t.c.

Kila app unayoipakua hasa social media apps zina security protocals zinazotofautiana hivyo ni vyema ukafahamu kabla hujauamini mtandao huo kwa taarifa zako. Account verifications au 2FA Itakusaidia sana wewe mtumiaji kuwaepuka wadukuaji kwa apps au social medias. Lakini pia kwenye email kuna verification ya kulinda password au kuepuka udukuaji kwa kuformulate maswali na majibu utakayoyajua wewe peke yako hivyo kutunza taarifa hizo sehemu salama kutawasaidia sana.

Pia tukwepe kitu kinaitwa Social engineering, yaani unatumiwa mtu (hasa wanawake hutumika) katika kufuatilia taarifa zako ili kufanikisha zoezi la udukuaji. Hivyo tuwe makini.

Am not a proffesional but i have concrete ideas of what the hell am doing. Linda Taarifa zako ili Zikulinde.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…