Umri sahihi kwa mtoto kuanza darasa la kwanza (Grade 1)

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
502
938
Wanajf, Salaam!!
Naombeni mnisaidie hasa kwa wale wataalamu wa Elimu ya watoto na saikolojia ya watoto. Umri gani ni mzuri kwa mtoto kuanza darasa la kwanza?

NITASHEREHESHA
nina mtoto wangu wa kike mwenye umri wa miaka mitano na miezi miwili. Anasoma Lower Kindergarten (Lower KG B). Ana uwezo wa kusoma maneno mepesi (simple words) kama mama, baba, cat, dog etc.

Ana uwezo wa kuhesabu na kufanya hesabu ndogo ndogo za kujumlisha (simple mathematics) mfano: 5+4=?,9+6=?, 3+2=?

Je, kwa umri huo wa miaka 5 ni muafaka kumuanzisha darasa la kwanza (Grade 1)? Au nimuache mwakani 2016 aingie Upper Kindergarten, na 2017 panapo majaaliwa yake Rabbana ndipo aanze darasa la kwanza (Grade 1)?

Ushauri wenu ndugu
 
....hao waliomuwezesha kuwa na uwezo wa kusoma na kufanya hesabu si ndio wameweka hizo Lower na Upper KG?
...huwaamini tena,ama?
 
Wanajf, Salaam!!
Naombeni mnisaidie hasa kwa wale wataalamu wa Elimu ya watoto na saikolojia ya watoto. Umri gani ni mzuri kwa mtoto kuanza darasa la kwanza?

NITASHEREHESHA
nina mtoto wangu wa kike mwenye umri wa miaka mitano na miezi miwili. Anasoma Lower Kindergarten (Lower KG B). Ana uwezo wa kusoma maneno mepesi (simple words) kama mama, baba, cat, dog etc.

Ana uwezo wa kuhesabu na kufanya hesabu ndogo ndogo za kujumlisha (simple mathematics) mfano: 5+4=?,9+6=?, 3+2=?

Je, kwa umri huo wa miaka 5 ni muafaka kumuanzisha darasa la kwanza (Grade 1)? Au nimuache mwakani 2016 aingie Upper Kindergarten, na 2017 panapo majaaliwa yake Rabbana ndipo aanze darasa la kwanza (Grade 1)?

Ushauri wenu ndugu

Mkuu nadhani hata mimi ushauri utakaopewa unaweza kunifaa, mwanangu kwa sasa hivi ana miaka 6/6months, mwakani anaingia darasa la pili P2, maendeleo yake si mabaya hajawi kupata wastani wa 96% hapo darasani kwao akiwa kindergarten hadi hio P1.
 
Kwa miaka 5 alitakiwa awe tiyari Upper Kg kuna mahali umemchelewesha maana kuna ambacho angejifunza UKg.. kwa sababu maendeleo yake ni mazuri itabidi usirudie kosa tena kumchelewesha... miaka 5 ni umri mzuri kuanza grade 1.....
 
Aanze tu la kwanza,acha woga, kwani kwa nchi zilizoenfelea mtoto wa miaka 16 alishamaliza na degree inakuwaje. Kama yupo vizuri kichani aanze tu.mbona zamani hiyo chekechea haikuwepo. Mi mwenyewe sikusoma nilifundishwa nyumban na dada ambaye alikuwa la kwanza ye anaingia la pili mi nikaingia la kwanza na nikawabututa vixuri tu waliosoma chekechea for 2 years
 
Mpeleke haraka sana Grade One(Darasa la Kwanza). Kwa sababu.
1/Umri sio namba bali umri ni kukua na kukomaa. Namba ni kivuli tu cha umri wa mtu lakini namba sio umri halisi. Huyo mtoto wako tayari kiakili amekomaa barabara kuanza darasa la kwanza.

2/Mtoto wa Kike anakuwa haraka sana Kimwili na kiakili kulinganisha na mtoto wa kiume.

3/Kasi ya Kujifunza mtoto inakwenda kwa haraka sana kuliko hata mifumo ya Elimu iliyopo, hivyo usifungwe na kanuni za mifumo ya kutoa Elimu ambayo ni Formality tu. Cha msingi ni upeo wa mtoto.

4/Ni vyema mtoto akawahi kujifunza mambo mengi ya Kielimu angali akiwa bado mdogo kabla akili haijajazwa na ujana na pilikapilika za maisha hususani watoto wa kike.
 
Mi nilianza darasa la 1 nikiwa na miaka 5 miezi 9. Lakini mi nilikuwa najua vitu kibao kama majina ya marais wa dunia, mlima mrefu kuliko yote etc. Huwezi kunilinganisha na mwanao ambaye anaonekana kama kilaza tuuu. So jipange mkuu. Usitafute sifa za kumuingiza mapema shule halafu akarudi na ujauzito
 
Watanzania tunachelewesha watoto sana. Nilishaishi Harare, na kule niliona umri uliotangazwa wa kuanza darasa la kwanza ni miaka 5. Nimeona huo ndio umri unaotakiwa kwenye nchi nyingine pia.

Binafsi nilimwanzisha binti yangu darasa ka kwanza akiwa na umri mdogo. Aliingia UCT akiwa na miaka 16, akamaliza first degree, honours na Masters akiwa 21.

Topic hii mimeijadili kwenye mada hapa inayoitwa "Mediocrity in Education".
 
Atakuwa mzigo mtu kazini
 
Kwa umri huo alitakiwa awe upper kindergatern,Mwanangu ndo kafikisha five yrs mwezi huu na yupo upper kindergarten tangia September na September mwakani anaingia kwanza
 
Back
Top Bottom