Umoja wa vijana nje ya vyama vya siasa!

Umoja wa vijana nje ya vyama vya siasa!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,199
Reaction score
7,562
Wadau,

Kwa kuwa vijana wa Tanzania kama ilivyo vijana wengine duniani, tunakabiliwa na changamoto nyingi, na tunapaswa kufikiri na kuchukua hatua katika kutambua mustakabali wa hatma yetu kwa ujumla;Je!

1.Unadhani pamoja na jitihada za mtu mmoja mmoja, ipo haja ya kuwa na jumuia/umoja wa vijana kama majukwaa ya kujadili na kutafutia ufumbuzi matatizo yanayo wakabili vijana?

2. (a)Unadhani jumuia za vijana ndani ya vyama vya siasa (UVCCM, BAVICHA n.k) zinatoa mchango wa kuridhisha katika kuyatambua na kuyatatua matatizo yanayowakabili vijana nchini?

(b) Ni kwa kiasi gani unaridhishwa na michango ya jumuia hizi (za vijana ndani ya vyama)katika ku ya-address matatizo na changamoto zinazowakabili vijana?

3. (a) Unafikiri ipo haja ya kuwa na jumuia ya umoja wa vijana nje ya vyama vya siasa ambayo itawaunganisha vijana wote na kushungulikia matatizo yanayowagusa moja kwa moja bila kujali vyama vyao

(b) unadhani upo uwezekano wa kuwa na umoja wa aina hiyo?
(c) ungependa umoja huo uwe vipi kama ikitokea ukiwepo?

Kama unaweza kuwa na wazo lolote, tunaweza ku-share!

karibuni.
 
Kuna vijana wazee, we ni mmojawapo! mtu asiyejifahamu eti naye anajiita kijana!
 
Ni vizuri kuwa na Umoja wa Vijana lkn tatizo tulilokuwa nalo ni hao vijana kutoka ktk hizo taasisi ulizozitolea mfano. Wao wataweka maslahi ya vyama vyao mbele kuliko huo umoja. Uwezekano upo kwa wale vijana waliokuwa hawana vyama.
 
Hii kitu ni Muhimu lakini MACCM hawapo tayari kwa hili ndio maana Hawataki hata BARAZA LA VIJANA LA TAIFA.
 
Bado sana kuwa na Jukwaa la vijana la Taifa kwa sababu zifuatazo:--

1. Asilimia kubwa ya vijana bado hawajitambui, ujinga wa kukosa elimu... Hata hao waliofanikiwa kupata elimu bado fikra zao zimegubikwa na imani kuwa Serikali kuwawekea mazingira bora ya kujiendeleza ni hisani na si haki yao.. hali hiyo hupelekewa wao wachache kuwa wachumia tumbo kwa kutumiwa na utawala kwa ajili ya kufanikisha malengo ya watawala..

2. Wengi bado hajatambua kuwa matatizo ya kiuchimi na kijamii Tanzania ni kushindwa kwa Utawala wa CCM ulidumu kwa muda wa miaka 50.. Sasa huwezi kujitibu mpaka ujitambue kuwa unatatizo na tatizo hilo linahitaji Daktari wa kukutibu.. Mbaya zaidi kwa kutumiwa na watawala wanapumbazwa na fedha kutoka kwa watawala ili wasiendelee kudai haki za msingi...

3. Kwa historia na uzoefu hata hilo jukwaa likiwepo litahujumiwa kwa gharama yoyote na Serikali kwa kupandikiza watu wake ili kufifisha malengo waliojiwekea..

Acha tuendelee hivihivi mpaka vijana wenyewe watakapoamka kutoka usingizini na kudai mageuzi makubwa ya kimfumo na kiutawala... Nishauri tuendelee kuwaunga mkono wale wote wanaendeleza mapambo ya mageuzi nchini mwetu.. Hakuna ubishi kilichopo nchini ni vita kati ya Haki vs dhuruma, Uadilifu vs Ufisadi, Uzalendo Vs Ulafi, Uelewa Vs Ujinga na CHADEMA vs CCM..

Kazi kwako... Jitambue upo kwenye kundi gani..
 
Vijana wa Tanzania ni kama vile ama hatuna maono, au hatupendani.
 
Vijana wa Tanzania ni kama vile ama hatuna maono, au hatupendani.
Bavicha inatosha hao vijana wengine wa uvccm na ACT ukiwemo wewe ni wachumia tumbo tu mnanyemelea vyeo kwa kujikomba kwa mafisadi wa CCM.
 
Bavicha inatosha hao vijana wengine wa uvccm na ACT ukiwemo wewe ni wachumia tumbo tu mnanyemelea vyeo kwa kujikomba kwa mafisadi wa CCM.
ndio nauliza, hatuwezi kuwa na umoja nje ya vyama vya siasa? sijui umelewa hoja!?
 
Wadau,

Kwa kuwa vijana wa Tanzania kama ilivyo vijana wengine duniani, tunakabiliwa na changamoto nyingi, na tunapaswa kufikiri na kuchukua hatua katika kutambua mustakabali wa hatma yetu kwa ujumla;Je!

1.Unadhani pamoja na jitihada za mtu mmoja mmoja, ipo haja ya kuwa na jumuia/umoja wa vijana kama majukwaa ya kujadili na kutafutia ufumbuzi matatizo yanayo wakabili vijana?

2. (a)Unadhani jumuia za vijana ndani ya vyama vya siasa (UVCCM, BAVICHA n.k) zinatoa mchango wa kuridhisha katika kuyatambua na kuyatatua matatizo yanayowakabili vijana nchini?

(b) Ni kwa kiasi gani unaridhishwa na michango ya jumuia hizi (za vijana ndani ya vyama)katika ku ya-address matatizo na changamoto zinazowakabili vijana?

3. (a) Unafikiri ipo haja ya kuwa na jumuia ya umoja wa vijana nje ya vyama vya siasa ambayo itawaunganisha vijana wote na kushungulikia matatizo yanayowagusa moja kwa moja bila kujali vyama vyao

(b) unadhani upo uwezekano wa kuwa na umoja wa aina hiyo?
(c) ungependa umoja huo uwe vipi kama ikitokea ukiwepo?

Kama unaweza kuwa na wazo lolote, tunaweza ku-share!

karibuni.


Linapingw ausiku na mchana, kama ilivyopingwangwa umoja wa wanawake nje ya UWT enzi hizo.
 
Back
Top Bottom