Umoja wa Rufaa ya Wananchi (URUWA), waipongeza Serikali ya awamu ya tano

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,859
Wakati kukiwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umoja wa kisiasa unaounganisha vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, kumejitokeza umoja mwingine wa kisiasa wa kivyama. Umoja huo ni Umoja wa Rufaa ya Wananchi (URUWA) unaoundwa na vyama visivyopata ruzuku ya Serikali: Ada-TADEA, UDP,UPDP na SAU.

URUWA jana umeunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli. Umoja huo uko chini ya Katibu Mkuu wa Ada-TADEA, Ndugu John Magale Shibuda. Namuona Shibuda akijaribu kutoka kivingine baada ya kuhama kutoka CHADEMA na kupoteza hata nafasi yake ya Ubunge katika Jimbo lake la Maswa Magharibi.

Siasa za Tanzania zimekuwa za kuigana sana. Kuigana kulikolea kwenye kampeni ambapo M4C ilitumiwa na CHADEMA pamoja na CCM. Wakati CHADEMA wakimaanisha Movement for Change, CCM walimaanisha Magufuli for Change. Sasa URUWA imechomoza ikiwa na mwitiko wa UKAWA na URUWA yaweza kuibuka na mgombea mmoja kwenye chaguzi. Siasa za Tanzania zina vituko sana.

================================

URUWA YAIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

Mwenyekiti wa Umoja wa Rufaa ya Wananchi (URUWA) John Shibuda(katikati) akisistiza jambo kwa waandishi wa Habari wakati umoja huo walipokuwa wakitoa pongezi kwa Rais wa Awamu ya Tano

Na Lilian Lundo MAELEZO

Uongozi unaounda mashirikiano ya umoja wa vyama visivyo na Ruzuku ya Serikali ambavyo ni ADA-TADEA, UDP, UPDP na SAU uitwao URUWA (Umoja wa Rufaa ya Wananchi) umeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uongozi uliojaa utukufu wa uzalendo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa URUWA John Shibuda leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongeo na waandishi wa habari.

?Tunamuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za utumishi aminifu na tiifu kwa ustawi na maendeleo ya Jamii na Taifa, hongera sana kwa uongozi wako uliojaa utukufu wa uzalendo na Neema ya kauli aminifu ya HAPA KAZI TU ambayo ipo kwa maslahi ya Tanzania,? alisema Shibuda.

Umoja huo pia umepongeza mshikamano wa uzalendo na uwajibikaji makini unaotekelezwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Shibuda aliongeza kwa kusema kuwa wananchi wa makundi yote yasiyotarajia kuingia katika kundi la uchumi wa kati sasa wanamatumaini ya kufikia uchumi wa kati kutokana na kupata utumishi sikivu kwa vilio vyao vya muda mrefu vya kupata maisha bora.

Aidha, uongozi wa umoja huo umesema kwamba unaunga mkono juhudi zote zinazotekeleza Serikali ya Awamu ya Tano katika kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jamii na Taifa. Pia wameitaka Serikali ya Awamu ya Tano kuendelea kutakatisha na kung?arisha usafi wa mazingira ya uwajibikaji wa safari ya ukombozi ya ASP na TANU.

Umoja wa vyama visivyo na Ruzuku ya Serikali URUWA umeundwa tarehe 18/12/2015 huku Mwenyekiti wa Umoja huo akiwa ni John Shibuda ambaye ni Katibu Mkuu- ADA-TADEA, Katibu Mkuu akiwa ni Fahami Nassoro Dovutwa ambaye ni Mwenyekiti Taifa ? UPDP.

Wajumbe wa umoja huo ni Isaac Cheyo ambaye Katibu Mkuu ? UDP, Paul Kyara Mwenyekiti SAU na Yusufu Manyanga ni Makamu Mwenyekiti ? SAU.

Chanzo: Sufianimafoto
 
Vyama vyote vilivyo chini ya URUWA ni agents wa CCM hapo wanamsubiri kaka yao ACT - WASALITI ili umoja ukamilike.
 
Kumbe mwenyekiti wake ni shibuda? Duh kweli kapoteza dira kaamua kuunda umoja huo ili aonekane
 
Uruwa!!! Hii inanionyesha ni kwa jinsi gani watu walivyokosa ubunifu. Inanikumbusha enzi za babu wa Loliondo alivyopata kick mara kikaibuka kikombe cha rombo, sijui bibi wa Tabora na upuuzi kama huo. Hii Uruwa imeundwa kwa ajili ya kujipendekeza ili kupata chochote toka serekalini, kwa bahati mbaya sana serekali hii ya Magufuli sio dhaifu kiihivyo kiasi cha kuhitaji kusifiwa kijinga hata kama inangependa kusifiwa. Hivi vikundi vilikuwa na maana sana wakati wa JK kwani vilitumika kama sehemu ya kuficha udhaifu uliokuwepo.
 
Huenda URUWA ikasimamia kile inachokipigania. UKAWA sijui kama bado wanasimamia kuwepo kwa Katiba yenye mapendekezo ya wananchi ambayo inataka uadilifu wa viongozi na kupinga ufisadi nchini!
 
Shibuda naye anahangaika kama msaliti mwenzake Zitto
 
Last edited by a moderator:
Hawa wampoteza mwelekeo. Wanatafuta sympathy ya Magufuli lakini hawapati kitu. Badala ya kujenga vyama vyao ili wapate angalau viti vya ubunge mwaka 2020, wanapoteza muda kwa kuitisha press coneferences!
 
Wakati kukiwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umoja wa kisiasa unaounganisha vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, kumejitokeza umoja mwingine wa kisiasa wa kivyama. Umoja huo ni Umoja wa Rufaa ya Wananchi (URUWA) unaoundwa na vyama visivyopata ruzuku ya Serikali: Ada-TADEA, UDP,UPDP na SAU.

URUWA jana umeunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli. Umoja huo uko chini ya Katibu Mkuu wa Ada-TADEA, Ndugu John Magale Shibuda. Namuona Shibuda akijaribu kutoka kivingine baada ya kuhama kutoka CHADEMA na kupoteza hata nafasi yake ya Ubunge katika Jimbo lake la Maswa Magharibi.

Siasa za Tanzania zimekuwa za kuigana sana. Kuigana kulikolea kwenye kampeni ambapo M4C ilitumiwa na CHADEMA pamoja na CCM. Wakati CHADEMA wakimaanisha Movement for Change, CCM walimaanisha Magufuli for Change. Sasa URUWA imechomoza ikiwa na mwitiko wa UKAWA na URUWA yaweza kuibuka na mgombea mmoja kwenye chaguzi. Siasa za Tanzania zina vituko sana.

================================

Chanzo: Sufianimafoto

Washangaa siasa za kuigana Tz?
Huoni chadema walivoiga muundo wa kiutawala wa ccm na jumuia zake.
Bavicha imeigwa uvccm
Bawacha UWT
Muundo wa Mwenyekiti, Makamu, Makatibu, kamati kuu etc.
Wameiga sana tu.
 
Wakati kukiwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umoja wa kisiasa unaounganisha vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, kumejitokeza umoja mwingine wa kisiasa wa kivyama. Umoja huo ni Umoja wa Rufaa ya Wananchi (URUWA) unaoundwa na vyama visivyopata ruzuku ya Serikali: Ada-TADEA, UDP,UPDP na SAU.

URUWA jana umeunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli. Umoja huo uko chini ya Katibu Mkuu wa Ada-TADEA, Ndugu John Magale Shibuda. Namuona Shibuda akijaribu kutoka kivingine baada ya kuhama kutoka CHADEMA na kupoteza hata nafasi yake ya Ubunge katika Jimbo lake la Maswa Magharibi.

Siasa za Tanzania zimekuwa za kuigana sana. Kuigana kulikolea kwenye kampeni ambapo M4C ilitumiwa na CHADEMA pamoja na CCM. Wakati CHADEMA wakimaanisha Movement for Change, CCM walimaanisha Magufuli for Change. Sasa URUWA imechomoza ikiwa na mwitiko wa UKAWA na URUWA yaweza kuibuka na mgombea mmoja kwenye chaguzi. Siasa za Tanzania zina vituko sana.

================================

Chanzo: Sufianimafoto
Sijui kwanini CDM imewekeza sana kwenye CHUKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.Yaani kwavile fulani hauko nae basi unapaswa kushawishi watu wakuchukie.Vyama vyote[uKIACHA ACT]Mfumo wao wa uongozi kwa maana ya muundo wameiga CCM.In short vyama vya upinzani vyote vinaiga CCM.Kuunganisha upinzani na nyie mmeiga wapi huko ambapo wengine hawapaswi kuiga??????????????????????
 
Back
Top Bottom