Umoja wa Mataifa waunga mkono uchaguzi wa rais Somalia

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,189
10,668
  • 4bk511e0e389f36wid_800C450.jpg
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema linaunga mkono kikamilifu mpango wa kufanyika uchaguzi mkuu nchini Somalia.

Baraza hilo limesema liko tayari kuunga mkono kwa hali na mali, uchaguzi wa rais nchini Somalia, unaotazamiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Taarifa ya baraza hilo imeongeza kuwa, maeneo mengi ya nchi hiyo kwa sasa yanashuhudia usalama na amani na kwamba uwepo wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini humo AMISOM, kumezaa matunda kwa kiasi kikubwa. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatazamiwa kutembelea Somalia kati ya leo na tarehe 21, kuonyesha uungaji mkono wao kwa uchaguzi huo.

Uchaguzi huo utakuwa wa pili tangu vita vya ndani vianze katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika mwaka 1991, ikizingatiwa kuwa uchaguzi mwingine ulifanyika mwaka 2012.

Itakumbukwa kuwa, baraza la mawaziri na viongozi wa kitaifa wa Somalia katika kikao chao cha Januari 28 mwaka huu katika mji mkuu Mogadishu, waliafiki kuwa, baraza la mawaziri litavunjwa kabla ya uchaguzi ili kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi wa rais na wa bunge.
 
Back
Top Bottom