Umoja wa Mataifa (UN) umeipongeza Serikali ya Tanzania kwa namna inavyotumia vizuri rasilimali zake

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1566461153925.png


UMOJA wa Mataifa (UN) umeipongeza Serikali ya Tanzania kwa namna inavyotumia vizuri rasilimali zake za ndani na hivyo kuiwezesha kutekeleza shughuli mbali mbali za kimaendeleo, na kupunguza utegemezi kutoka nje.

Pongezi hizo zimetolewa jana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, osini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam. Rodriguez alikwenda kumuaga Waziri Mkuu, alisema Tanzania imeendelea kutumia vizuri mapato yake ya ndani kwa kuimarisha miundombinu na huduma za kijamii kama ujenzi wa hospitali na vituo vya afya.

“Katika kipindi changu cha miaka mitano ambacho nimefanya kazi Tanzania, nimeshuhudia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayofanywa na serikali, ikiwemo kuimarika kwa mahusiano kati ya serikali na Umoja wa Mataifa na taasisi zake nchini,” alisema Rodriguez. Katika hatua nyingine, Rodriguez ameisifu Serikali ya Tanzania kwa namna ilivyoandaa na kuendesha vizuri Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Agosti 17 na 18, mwaka huu.

Mbali na kuisifu serikali pia kiongozi huyo amevipongeza vyombo vya habari kwa jinsi vilivyoshirikiana na serikali kuripoti matukio mbali mbali ya mkutano huo. “Nawapongeza na wananchi kwa ushirikiano walioutoa kwa serikali wakati wote wa mkutano wa SADC,” alisema. Kwa upande wake, Waziri Mkuu alimshukuru kiongozi kwa pongezi alizozitoa ambazo ni ishara kwamba anatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli katika kutumia vizuri rasilimali zake.

Waziri Mkuu alisema “maelezo yaliyotolewa na Bwana Rodriguez yanaakisi kauli za Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwamba Tanzania si nchi masikini na inayo uwezo wa kutoa misaada kutokana na rasilimali nyingi ilizonazo. Watanzania waendelee kuiunga mkono serikali yao,” alisema Waziri Mkuu.

Pia, alitumia fursa hiyo kumpongeza kiongozi huyo kwani alikuwa kiungo kizuri baina ya Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa. Pia atakumbukwa kutokana na mambo mengi aliyoyafanya kipindi cha utumishi wake nchini. Awali, Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini, Balozi Thamasanqa Mseleku ambaye alikwenda kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini.

Waziri Mkuu alimpongeza balozi huyo kwa ushirikiano na mchango alioutoa kwa Serikali ya Tanzania katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo zikiwemo za kiuchumi, elimu, afya, maendeleo ya jamii pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya nchini mbili hizo. Kwa upande wake, Balozi Mseleku aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa uliompatia katika kipindi chake cha utumishi akiwa nchini, na alitamani aendelee kubaki Tanzania.
 
Tukutane 2020 mtueleze mmefanya nini miaka mi 5. Siku hizi ile lugha ya viwonder imeyeyuka na sasa mmeegemea kwenye pongezi. Hivi wale waunga juhudi wameishia wapi? Au siku hizi juhudi hazipo?
 
Siku hizi wamesahau mpaka msemo wao uchwara wa hapa kazi tu.
Tukutane 2020 mtueleze mmefanya nini miaka mi 5. Siku hizi ile lugha ya viwonder imeyeyuka na sasa mmeegemea kwenye pongezi. Hivi wale waunga juhudi wameishia wapi? Au siku hizi juhudi hazipo?
 
sisi wapiga kura safali hii tutapiga kura na kuzilinda kwa nguvu zote, tutajumlisha matokeo ya urais kutoka kila kituo wenyewe, sasa ole wao NEC walete mazingaombwe yao, damu itamwagika! hatuwezi kuvumilia huu ubabaishaji kwa miaka mingine 5.
 
Back
Top Bottom