Alianza na watumishi wa umma akawatengua bila makosa, watu wengi walishangilia kitendo hicho na kumsifia, bila kujali kuwa Watanzania wenzetu wengi walikuwa wakionewa bila kosa aidha kwa chuki binafsi.
Akaja kwa vyama vya siasa, akazuia shughuli zao ambazo zipo kwenye katiba ikiwemo mikutano ya hadhara, wananchi wakakaa kimya, vyombo vya habari vikakaa kimya wala hakukemewa hata viongozi wa dini kuhusu mwenendo wake huo wa siasa.
Amezuia ajira serikalini, vijana wamebaki wakilia vilio vya samaki hawajui kushoto yao lakini jamii umewaacha wakilia bila msaada si viongozi wa dini wala wananchi wanahoji kuhusu hilo ni kwa vile haliwagusi moja moja.
Ameteka bunge, bajeti anapanga yeye, sheria anatunga yeye wabunge wetu wamebaki kimya wanatumika hawajitambui na wala hawahoji mamlaka hiyo alipoitoa kwa vile hawajaguswa.
Kipindi anatumbua wananchi huko vijijini walimshangilia bila kujua kwamba wengi walitumbuliwa sababu ya visasi na chuki leo hii wanalia njaa kaziba pamba masikioni na kasema hatoi chakula cha msaada ng'o, wameguswa.
Magazeti nayo yameguswa, watumishi wa umma wameguswa, wahitimu vyuo vikuu wameguswa, wananchi wenye njaa wameguswa, wafanyabiashara wameguswa.
Wamebaki viongozi wa dini, mmeyafumbia macho haya yote hammkemei mtu huyu kwa kujiona mpo salama ipo siku mtaguswa.