Umeya waigawa CCM

Umeya waigawa CCM

Bintiwangara

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
551
Reaction score
287

[TD="bgcolor: #ffffff"]KUMEZUKA hali ya sintofahamu miongoni mwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa Tabora na uongozi wa CCM, baaada ya mwenyekiti wa chama mkoa, Hassan Wakasuvi, kuahirisha uchaguzi wa naibu meya.

Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike Julai 31, mwaka huu, lakini haukufanyika ambapo nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na diwani wa kata ya Ipuli, Waziri Mlenda.
Licha ya uchaguzi huo kuahirishwa, hakuna taarifa yoyote ya mkoa iliyoonyesha ni lini utafanyika, zaidi ya kudaiwa kuwa kuna mipango ya kutaka kuchakachua wagombea wasiotakiwa na baadhi vigogo wa mkoa.
CCM wilaya ilipendekeza majina ya Musa Msamazi, Salum Luzila, Shaban Kaombwe, Alfonce Shushi, Waziri Mlenda na Ndaki ambapo ilipanga uchaguzi huo ufanyike Julai 31 mwaka huu.

Baadhi ya madiwani wamelidokeza gazeti hili kuwa Wakasuvi ameahirisha uchaguzi huo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa kuna mgombea mmoja alikuwa hamtaki na hivyo kutaka kuchomeka chaguo lake.
Kutokana na hilo, baadhi ya madiwani wamesikika wakitamka kuwa ipo siku viongozi hao wa mkoa watakiingiza chama kwenye mgogoro usioisha kutokana na ubinafsi wao kwenye uchaguzi.

Inadaiwa kuwa ndani ya CCM mkoa kila kiongozi ana mtu wake katika mbio hizo za uchaguzi wa naibu meya, ambapo mstahiki meya wa manispaa hiyo, Ghulam Remtulah, akidaiwa kumbeba diwani wa Ikomwa, Musa Msamazi, japo amekana tuhuma hizo.



[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Mwandishi wetu, Tabora



[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff"][/TD]

[/TD]
 
Safi sana, vita vya panzi, furaha ya kunguru...acha wagombane vizuri ili watutengenezee njia ya ikulu na majimbo yoote.
 
Yaleyale ninayosema cku zote viongozi CCM wamekwisha wamebaki waloho wamadalaka,majizi majangili,wauza dawa za kulevya pamoja na wauaji tu.
 
Ndo kazi yao, wako wenyewe na bado wanaendeleza yaleyele ya ukoo wa panya
 
Zungumzia umeya wa mwanza na ilemela acha kuweweseka kwa vihabari uchwara
 
Kiwia na meya matata ndio habari ya mjini kuhusu migogoro ya mameya
 
Back
Top Bottom