Umewahi kukesha bila kufumba hata jicho usiku kucha mpaka unaliona jua tena!

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,744
Hii kitu isikie tu, nilikuwaga siamini kama mtu anaweza tembea huku amesinzia.

Kumbe ni kweli aisee kipindi hicho tulikuwa tunaenda madrassa usiku na tuna kesha na asubuhi tunaenda shule kama kawaida

Kuna siku ikitokea kuna harusi au dua tunaenda kukesha kwa kuimba na kupiga dhikri,

Mwalimu wetu alikuwa mkali sana yaani ukisinzia tu anakupiga na tambo au mkanda mgongoni,

Hivyo ilikuwa ni ngumu kumuona mtu anasinzia kabisa

Sasa kwasababu tulikuwa tunatembeaga sehemu mbali mbali, siku moja tunarudi mida ya saa 11 kuna mwenzetu mmoja akawa anasinzia huku anatembea na amefumba macho kabisa tukawa tunamuangalia huku tunamcheka maana alikuwa katikati ya kundi, hii sijui ilitokeaje na wala hajikwai kabisaa.

Sent from my TECNO CA8 using JamiiForums mobile app
 
Nilienda kwa mganga baada ya kuoga mara saba na kufukizwa mara nne kwa masaa 8 nikajua tayari nikapelekwa kwenye kiti Kuchanjwa hapo saa 1 kasoro nikajua tayari mara naambiwa ukifika nyumbani hamna kulala hadi jua lichomoze ndo ulale alo kufika alfajiri bila energy nilikuwa sitoboi
Baada ya mateso yote hayo ulifanikisha kilichokupeleka kwa mganga?
 
umenikumbusha 2022 hii ndio ya utu uzimani.
NI 3 months mara baada ya ku deploy software yangu rasmi na kuanza kuwa ile effective ikitumika na taasis kadhaa.Hiyo siku nilipiga kazi for 28 hours non-stop ku fix technical complications users walizokua wanakutana nazo. 28 hrs umekaa tu mbele ya Laptop.

Nilikua peke yangu bado ndio nimeanza anza so nilikua napokea simu kama niko call centre. I remember niliingia mzigoni saa 4 asubuh mpaka kesho yake saa 7 mchana ndio nikarud home kupumzika.

But i was enjoying to do that. I always enjoy.
 
Back
Top Bottom