Umewahi kujiuliza vitu hivi

Gpaghy

Member
Sep 25, 2021
47
138
SOMO: PARADISO, KUZIMU, JEHANUM/ZIWA LA MOTO, MBINGU MPYA, NCHI MPYA, MIAKA 1000, YERUSALEM MPYA

Bwana Yesu Asifiwe karibu tujifunze tena, Tumaini la mkristo yeyote yule ni siku moja aende mbinguni, leo tujifunze vyitu hivyi ambavyo ni mhimu sana kuvijua

KWA NINI MWANADAMU ANAKUFA?
mwanadamu anakufa kwa sababu ya dhambi ya kuasi kwa adam na hawa!
Mwanzo 3:19
kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

JE, MWANADAMU AKIFA ANAENDA WAPI?
Mwanadamu yeyote anapofariki Roho yake hutoka nje ya mwili na kuvaa mwili mpya usioharibika tena
1 Wakorintho 15:53
Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.

Baada ya Roho kuvalishwa mwili mpya haya ni maeneo ambayo unatakiwa kwenda
1: KUZIMU, ni mahali ambapo wanaenda watenda dhambi tu / wasiompokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao
Luka 16:23
Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

SIFA MBAYA ZA KUZIMU
i: ni sehemu ya kutisha
Ii: ni sehemu yenye mateso ya kila aina
Iii: ni sehemu isiyo na matumaini
Iv: ni makao ya shetani, mapepo no
V: ni sehemu yenye moto japo mapepo na shetani hauungui wanaungua tu wanadamu waliopo hapo
Vi: waliopo kuzimu wanasubiri siku ya hukumu watupwe ziwa la moto

2: PARADISO YA MUNGU
Hii ni sehemu wanayoenda watakatifu kupumzika baada ya taabu zao ili kusubiri Siku ya hukumu
Luka 16:22
Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
Ufunuo wa Yohana 14:13
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

SIFA YA PARADISO
1: ni bustani ya Mungu mwenyewe
2: ni watakatifu tu wanaruhusiwa eneo hilo
3: Hamna mateso eneo hili ni raha tu

UNYAKUO
unyakuo ni kurudi kwa Yesu duniani ambako kutafanyika ghafula kufumba na kufumbua watakatifu wataondolewa duniani, wakati wa unyakuo, parapanda itapigwa na Yesu maenyewe atashuka mawinguni na watakatifu watamlaki huko, hii parapanda ni watakatifu tu wataisikia,
1 Wakorintho 15:52
kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

1 Wathesalonike 4:15
Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.

1 Wathesalonike 4:16
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

1 Wathesalonike 4:17
Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

MATUKIO MAWILI YATAKAYOTOKEA WAKATI WA PARAPANDA YA UNYAKUO
1: wafu waliokufa katika kristo( waliopo sasaivi paradiso) watafufuliwa kwanza
2: walio hai walio watakatifu wataungana wote kwa pamoja na watamlaki Yesu mawinguni

BAADA YA UNYAKUO NINI KITAENDELEA MBINGUNI
baada ya watakatifu kunyakuliwa wataenda mbinguni kwenye karamu ya mwanakondoo kula na kunywa pamoja na Yesu mwenyewe, kipindi hiki kitachukua miaka 7 hesabu ya duniani,
Ufunuo wa Yohana 19:9
Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.

Mathayo 8:11
Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;

BAADA YA UNYAKUO NI NINI KITAENDELEA DUNIANI( KWA WALIOBAKI)
baada ya unyakuo duniani itakuwa ni dhiki kuu ya kutisha ambako mpiga kristo atapewa mamlaka ya kutawala, hizi ni sifa mbaya za dhiki kuu
1: mpiga kristo ndiye atakuwa kiongozi wa dunia
2: kifo kitakuwa mkononi mwa mpiga kristo, hutakufa mwenyewe mpaka akuue yeye
3: hutanunua wala kuuza bila kuwa na 666
Ufunuo wa Yohana 13:16
Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;

Ufunuo wa Yohana 13:17
tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

Ufunuo wa Yohana 13:18
Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.

UTAWALA WA MIAKA 1000
baada ya dhiki kuu, Au miaka 7, Yesu mwenyewe atashuka kutoka mbinguni akiwa amepanda farasi,pamoja na watakatifu kila mmoja amepanda farasi atashukia sehemu ile ile aliyoondokea duniani,
Matendo ya Mitume 1:11
wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Ufunuo wa Yohana 19:11
Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

Ufunuo wa Yohana 19:12
Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

Ufunuo wa Yohana 19:13
Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

Ufunuo wa Yohana 19:14
Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

Ufunuo wa Yohana 19:15
Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

Ufunuo wa Yohana 19:16
Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

BAADA YA YESU KUSHUKA MATUKIO HAYA YATAFANYIKA
1: mpiga kristo atakamatwa atatupwa kwenye ziwa la moto pamoja na nabii wa uongo wakiwa hai
Ufunuo wa Yohana 19:11
Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

Ufunuo wa Yohana 19:12
Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

Ufunuo wa Yohana 19:13
Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

Ufunuo wa Yohana 19:14
Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

Ufunuo wa Yohana 19:15
Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

Ufunuo wa Yohana 19:16
Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Ufunuo wa Yohana 19:20
Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;

2: wafuasi wa mpinga kristo ambao walienda kwa ajili ya kuuangamiza israel/yerusalem watauliwa kwa upanga na malaika wapanda farasi na nyama yao italiwa na ndege
Ufunuo wa Yohana 19:11
Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

Ufunuo wa Yohana 19:12
Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

Ufunuo wa Yohana 19:13
Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

Ufunuo wa Yohana 19:14
Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

Ufunuo wa Yohana 19:15
Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

Ufunuo wa Yohana 19:16
Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Ufunuo wa Yohana 19:21
na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.
Baada ya ushindi huu wayahudi watamwamini Yesu maana amewashindia, hapa ndo ahadi ya Yesu kutimia ya kuwakumbuka israeli

3: shetani atafungwa miaka 1000 asitoke tena kuwadanganya watu
Ufunuo wa Yohana 20:2
Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;

3: Hukumu ya watakatifu wote itafanyika kwa ajili ya kila mmoja kupata ujira wake

Ufunuo wa Yohana 20:4
Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.

4:baada ya hapo wale waliouawa na mpinga kristo baada ya kuikataa kuipokea 666, watafufuliwa wataungana na watakatifu waliotoka mbinguni kutawala miaka 1000!
Ufunuo wa Yohana 20:4
Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.

Ufunuo wa Yohana 20:5
Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.

Ufunuo wa Yohana 20:6
Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.

Note: hii miaka 1000 watatawala watakatifu na hao waliosalia walio ambao walikubali kuipokea chapa ya 666, isipokuwa wafu wote wenye dhambi bado watakuwa hawajafufuliwa mpaka hapo
UTOFAUTI KWENYE UTAWALA HUU KATI YA WATAKATIFU NA WENYE DHAMBI( WENYE666) MAANA WOTE WATATAWLA NA YESU
1: wale wenye dhambi au 666, watakuwa bado wanaishi kimwili hivyo wataoa na kuolewa na watakuwa wengi
2: watakatifu watakuwa hawana hisia hivyo hawataoa watabaki kama walivyo
3: kipindi hiki hakutakua na kifo,njaa, huzuni, kilio itakuwa ni raha tu kwa sababu Mungu mwenyewe ndiye atakuwa kiongozi
KWA NINI UTAWALA WA MIAKA 1000???
Baada ya adamu kupoteza bahati pale bustanini, sasa Mungu anakuja kuwaonyesha njinsi gani alitaka kukaa na wanadamu kama nyoka asingemdangaya Eva! Utawala huu wa miaka 1000 wa Mungu mwenyewe hakutakuwa, na serikali yoyote , wala shule,wala hospitali, wala mashamba kila kitu ukitakacho unakipata Automatically

SHETANI ANAFUNGULIWA KUWADANGANYA TENA WANADAMU( WALE WALIO NA 666)
baada ya miaka 1000 kuisha shetani atafunguliwa ili awadanganye wanadamu na kumbuka kipindi hiki watakuwa wamezaliana watakuwa wapo wengi, na kwa sababu wapo kimwili watashawishika wataungana na shetani kwenda kupigana na Mungu, na Mungu atawashinda
Ufunuo wa Yohana 20:4
Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.

Ufunuo wa Yohana 20:5
Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.

Ufunuo wa Yohana 20:6
Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.

SHETANI BAADA YA KUSHINDWA VITA HII ATAKUWA WA 3 KUTUPWA KWENYE ZIWA LA MOTO
Ufunuo wa Yohana 20:7
Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;

Ufunuo wa Yohana 20:10
Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

HUKUMU YA MWISHO
baada ya shetani kutupwa kwenye ziwa la moto ndipo wafu wote, waliokufa tangu kuumbwa kwa dunia watafufuliwa, na watahukumiwa kila mmoja makosa yake, hapa kila mmoja atapita mbele ya hukumu atasomewa mashitaka yake
Ufunuo wa Yohana 20:7
Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;

Ufunuo wa Yohana 20:11
Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.

Ufunuo wa Yohana 20:12
Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

Ufunuo wa Yohana 20:13
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Ufunuo wa Yohana 20:14
Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

Ufunuo wa Yohana 20:15
Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

YERUSALEMU MPYA
haya ni makao ya watakatifu milele
Ufunuo wa Yohana 21:2
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

Ufunuo wa Yohana 21:3
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
 
Back
Top Bottom