Umewahai kuwaza kitu hiki?

Umewahai kuwaza kitu hiki?

Reality of heaven

Senior Member
Joined
Nov 2, 2022
Posts
108
Reaction score
353
Habari wapendwa? Kuna kitu kinaitwa Ziwa la Moto, umewahi kuwaza kitu hiki?

Ziwa la Moto ni mahali watakapotupwa watenda dhambi wote kwenye hukumu ya mwisho pamoja na shetani na malaika zake( majini /mapepo)

Ufunuo wa Yohana 21:8, Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

SIFA ZA ZIWA HILI LA MOTO
1. Ziwa hili Moto wake ni mweusi sio kama huu wa duniani (Mathayo 25:30
Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno)

2. Moto wa ziwa hili ndani yake Kuna funza wenye meno ambao watawatesa wanadamu milele na milele (Marko 9:45) Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum.

Marko 9:46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.

3. Watakaoenda kwenye ziwa hili la Moto watateswa usiku na mchana wala hawatapumzika Wala hawatakufa maana kifo hakitakuepo

Ufunuo wa Yohana 14:11a
Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku

Namna ya kuepuka mahali hapa
1. Mwamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. Yohana 3:36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

2. Ishi maisha matakatifu, (acha wizi wa Mali ya umma, ufisadi, uongo, uzinzi, uchawi, uganga, wivu, hasira, samehe, qcha kupendelea)

Zaburi 16:3
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.

Uwe na siku njema! Karibu kwenye tafakuri hii ya leo
 
Back
Top Bottom